dikteta2020
JF-Expert Member
- Aug 14, 2018
- 595
- 3,991
Huu ni ushauri wangu wa dhati na wa kweli kwa Rais Magufuli na CCM wote. Magufuli aache kupiga kampeni.
Nasema hivyo kwa sababu naamini kuwa kadiri anavyozidi kupiga kampeni wapo wapiga kura lukuki anawapoteza kirahisi kabisa. Nasema ukweli na ndivyo ulivyo.
Aidha kama atalazimika kuendelea kupiga kampeni basi asionyeshwe live! Kumuonyesha live kunapoteza kura nyingi sana ambazo angezipata kwa watu kutokusikiliza baadhi ya maneno kutoka kwake ambayo kimsingi yanavunja moyo.
Mzaha anaofanya kwenye kampeni huku akijua fika kuwa wapo walioumizwa na utawala wake kunazidisha kutokukubalika na kutakuwa na madhara makubwa kwenye sanduku la kura.
Huu ni ushauri wangu japo ni mfupi ila mwenye macho na auone, mwenye masikio na ausikie na mwenye mikono aufanyie kazi.