Ushauri wangu kwa Ndugu zangu WAISLAM

Ushauri wangu kwa Ndugu zangu WAISLAM

somijo

Senior Member
Joined
Apr 14, 2012
Posts
110
Reaction score
47
Kutokana na hali ya sintofahamu iyojitokeza hivi karibuni ya mauaji ya viongozi wa dini ya kikristo,(mchungaji Mathayo kule buseresere, padri Mushi kule Zanzibar na kupigwa risasi kwa kwa padri Ambrose Mkenda) pamoja na kumwagiwa tindikali kwa kiongozi wa dini ya kiislam (Shekhe Fadhir Suleiman), na katika yote dini ya kiislam ikihusihwa moja kwa moja na vitendo hivi. Sasa nadhani ni wakati muafaka wa waumini wa kiislamu kuujulisha umma kuwa dini ya kiislam kama dini haifundishi mtu kuua au kulipiza kisasi kama shekhe Ilunga na wenzake wanavyofundisha. Muandae maandamano ya aman kulaani vitendo hivi, lakini vile kuhusishwa kwa dini yenu na vitendo hivi, muonyeshwe kuwa kweli mmeguswa na haya mambo yanayoendelea na dini yenu kama dini haihusiki na unyama huu ila ni kikundi cha wahuni, magaidi kama akina Ilunga, ndo wanawachafulia dini yenu na mtoe wito kwa serikali kuwashughulikia wote wanachochea fujo kwa kigezo cha udini mara moja hasa kwa kuwachochea waislamu wawachukie wakristo na vile vile wakristo kuwachukia waislamu.
Jamani sisi ni ndugu, na ndo maana kwenye nyumba ya mwislamu anapanga mkristo na kwenye nyumba ya mkristo anapanga mwislam.
Kama ni paradiso/peponi au jehanamu si mkristo au mwislamu, wote vyatuhusu.
Kwa hiyo ndugu zangu Waislamu andamaneni.
 
Back
Top Bottom