Ushauri wangu kwa Rugemalila na ndugu zake Wafanye yafuatayo

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
  • Mzee pole sana lakini chukua tahadhari hususani magonjwa ya corona uraiani yanatisha
  • Mshukuru Mungu kwa kukuondoa mahabusu kimya kimya usifanye sherehe
  • Tenga mda wako ujitenge na wageni wenye huruma za kinafiki ikiwezekana.
  • Fanya kama lowassa, Jiepushe na vurugu za siasa wala usicoment chochote
  • Kuwa makini sana na shughuli za kijamii utakazoalikwa ikiwezekana chukua tahadhari kubwa!
  • Usipende sana kucheza na wajukuu kwasasa, ikilazimika hakikisha wajukuu wako salama (wametakasika) kabla ya kukumbatia!
  • Usiwaze kuanzisha biashara mpya kwa sasa kasimisha majukumu yako ili ujiepushe na stress zozote!
  • Kuwa mtu wa ibada, kula vizuri, kazi za bustani Fanya mwenyewe ili kuupa mwili mazoezi!
Hakuna Bure isiyokuwa na Bure ndani yake!
Awamu ya NNE iliyokufanya ukae mahabusu awamu ya TANO sasa imekupambania awamu ya SITA umetoka!

Karibu sana uraiani mzee RUGEMALILA lakini upepo umekoregeka ndiyo maana tunavaa barakoa!
 
Nchi hii kuja kuendelea ni ngumu sana
Nusu ya viongozi CCM walitakiwa wawe jela, lakini hakuna wananchi wanaojali.
Rugenalira alichukua pesa kweli na aligawana na viongozi wengi wa serikali. Cha kushangaza alikamatwa peke yake huku viongozi wa serikali wakilindwa.
Mbaya zaidi
kwa makusudi ushahidi ukawa unacheleweshwa tu.
 
Mzee ajiachie tu mbaya wake alishatangulia kuzimu Hakuna mwenye shida nae kwa sasa.
Hii Dunia sote ni wapitaji mengine ni kuukimbiza upepo tu
 
Mzee ajiachie tu mbaya wake alishatangulia kuzimu Hakuna mwenye shida nae kwa sasa.
Hii Dunia sote ni wapitaji mengine ni kuukimbiza upepo tu
Ndo anapeta sasa
 
[emoji15]kumbe ameshatoka sasa mbona imekua kinya2 sana mtu maarufu sana yule
 
Unafiki unakusumbua
 
Reactions: Auz
Ushauri mzuri. Pia natumaini atazingatia suala la kufanya Full Medical Check-up ili kujua hali yake ya kiafya kwa ujumla.
 
"China Mafisadi wanadhibiwa, huku Mafisadi wamekuwa kama Inspiration....."

Maneno ya mlevi mmoja alisikika akisema, baada ya hapo akamalizia "Mtanikumbuka...............".

Hapo ndipo nami nikagundua tuna safari ndefu sana kukijenga kuzazi chenye uchungu, uzalendo na uaminifu kwa taifa hili kwa manufaa ya kizazi kijacho, yaani unashangaa mpaka wale waliomponda kwa miaka mitano mfululizo kwenye majukwaa na kwenye magazeti yao ya kwamba mwizi, leo wanadai alionewa. Kweli yule mlevi alikuwa sawa "MTANIKUMBUKA ".
 
Kuna asichokijua kati ya haya? Kwenye siasa, sijawahi kuona anashabikia lolote, sembuse sasa!
 
Walipaswa hadi viongozi wa dini waliokula ile pesa wawe ndani
 
Hakika Mzee Ameteseka wakati Wapo Waliokula Nae hizo PESA lakini JELA Kateswa Yeye
Nimefurahishwa Sana na KITENDO cha Kutoka Mahakama ya KISUTU na Kwenda KANISANI kabla ya NYUMBANI Naamini Alikwenda Kumshukuru MUNGU na KUWASHTAKI wote Waliomfikisha Hapo
A
Hasira ya MUNGU lazima iwapate Wahusika Wote

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Heri lingefia korokoroni fisadi hili papa kama Mengi. May you perish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…