Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 349
- 805
Ushauri wangu kwa Vyombo vya ulinzi na usalama ni kwamba, kufanya ukatili sio kuogopeka. Zaidi, ni kuzidi kudharaulika na kuonekana hamna weledi wala hamjui majukumu yenu.
Mtu anayeogopeka ni yule anayewajibika. Mtu asiyepindisha. Mtu aliyenyooka. Hujawahi kukaa mahali ukasikia "Yule jamaa kanyooka sana. Hapindishi maneno." Hii ndio aina ya watu wanaoheshimika na kuogopeka kwasababu wanajali taratibu na kanuni bila kumuangalia mtu usoni.
Mnaweza kuendelea kunyanyasa wananchi ili kuwatia hofu lakini hilo halitafanya muogopeke. Ndio maana tangu matukio haya ya kikatili yaanze, watu hawajawahi kuacha kuzungumza. Zaidi, hata wale wasiokua waongeaji nao wameshindwa kukaa kimya. Bubu kanena kwa uchungu wa mwana.
Tumieni mafunzo yenu na ujuzi wenu kulinda amani na usalama wa taifa hili. Sheria imewapa nguvu kubwa mno. Ukimpigia mtu simu afike kituoni, bila shaka atafanya hivyo. Haina haja ya kumuendea mtu na mitutu kwaajili ya kumteka. Mathalani kwa ustaarabu aliokua nao Kombo Mbwana, mngempigia simu tu afike kituoni hapo Handeni angefanya hivyo. Hakukua na haja ya kumteka na kukaa nae siku 29 kwa kisingizio kwamba ana usajili wa laini usiokua wake. Hamuwezi kutufanya watanzania milioni 60+ wote wajinga kwa wakati mmoja.
IGP mstaafu Simon Siro aliwahi kusema kwamba ukifanya mambo ya hovyo kwasababu una mamlaka uliyonayo, wenye weledi wanakuona mpumbavu tu. Heshima haitafutwi kwenye mabavu. Inapatikana kwa kuwajibika. Jifunzeni kwa CDF wastaafu MWAMUNYANGE na MABEYO
Wajibika Uheshimike!