Aliko Musa
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 209
- 315
Imekuwa ni ndoto ya wengi kumiliki nyumba ya kuishi hasa kwetu sisi watanzania. Ndoto hii inaweza kutokana na sababu mbalimbali.
Kwenye kipengele hiki cha kumiliki nyumba ya kuishi nimekuandalia somo ambalo nimeona litakusaidia sana sana kuhusu nyumba ya kuishi.
Ninafahamu kuwa ushauri huu sio wa kila mtu anayesoma somo hili. Lakini ni moja ya maeneo ambayo yatamsaidia sana yule ambaye anahitaji kumiliki nyumba ya kuishi na familia yake.
Somo hili nimeliandaa baada ya kujifunza HAMASA ZA WAUZAJI kutoka kwenye vyanzo tofauti tofauti. Hivyo nimetumia ile kanuni yangu isemayo;-
✓ Ni lazima ununue nyumba/kiwanja kutoka kwa muuzaji aliyehamasika ili kutengeneza faida ya zaidi ya 20% wakati wa kununua nyumba/kiwanja hicho.
Pia, imeonekana kuwa wamiliki wengi wa nyumba za kuishi hawaendelii kuishi kwenye nyumba zao za msingi (primary residence) ndani ya miaka 7 hadi 9.
Bofya hapa kujiunga na mafunzo ya kujenga/kutunza utajiri kupitia ardhi na majengo.
House Hacking.
Hii ni mbinu ya kutengeneza pesa kwa kutumia nyumba yako ya msingi (primary residence). Ni mchakato wa kutafuta njia za kuingiza kipato kwa kutumia nyumba yako ya kuishi na familia yako.
Kwa sababu wengi wamekuwa wakinipigia simu kuniuliza kuhusu kupangisha nyumba zao za kuishi. Hivyo, nimekuja na somo hili zuri kwao.
Somo lenyewe ni kila ukifikiria kumiliki nyumba ya kuishi hakikisha unakuwa na mawazo mawili; wazo la kibiashara na wazo la makazi ya familia.
Sababu 7 Za Kwanini Nyumba Yako Ya Kuishi Iwe Ya Kibiashara.
Moja.
Umri.
Wengi wanaanza kupangisha nyumba zao za kuishi baada ya umri wao kuwa mkubwa. Mtu anafikia uzee ndipo huanza kufikiria kupangisha nyumba yake kuishi.
Wazo hili linakuwa halina manufaa makubwa ya kifedha kwake endapo limekuja kama ajali. Hii ni kwa sababu zifuatazo;-
✓ Usanifu wa jengo husika (architectural styles).
✓ Eneo nyumba ilipo.
Mbili.
Maendeleo binafsi ya mmiliki wa nyumba.
Nyumba unayoiona leo kuwa ni nyumba ya ndoto yako ya kuishi sio nyumba itakayokufaa kesho. Hii ni inatokana na mabadiliko ya usanifu wa majengo duniani, mabadiliko ya kiasi cha kipato chako, mabadiliko ya hali ya hewa, na kadhalika.
Huenda nyumba ukaona haikufai ifikapo miaka 5, au 10 ijayo. Hivyo ili kuepuka kuwa na hamasa ya kuuza nyumba kwa bei pungufu, unatatakiwa kupangisha nyumba yako.
Tatu.
Kuhamishwa eneo la kazi.
Uhamisho wa kituo cha kazi inaweza kuwa ni hamasa ya kukufanya uuze nyumba yako au uipangishe. Hivyo, kuna kipindi hutaishi kwenye nyumba yako kwa sababu za ajira yako. Nyumba yako utaipangisha kipindi hiki.
Nne.
Kufilisika.
Unaweza kufilisika kutokana na sababu zinazoonekana kwa uwezo wa kibinadamu na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wa kibinadamu.
Hivyo rafiki yangu, kama wewe una kipato kikubwa sana na umejenga mifereji imara ya kuingiza kipato fikiria kufilisika.
Ni lazima itokee kwenye maisha yako, haijalishi itatokea lini na kwa namna gani. Kipindi ambacho umeyumba kiuchumi, nyumba yako ya kuishi itageuka kuwa chanzo cha kipato.
Ni nani ajuaye kuwa nyumba yako ya kuishi itakuwa ni mwanzo wa kuinuka tena?. Ni nani ajuaye kuwa nyumba yako ya kuishi itatumika kukusanya mtaji fedha wa kunusuru biashara zako zinazokaribia kufa?.
Tano.
Hamasa nyingine.
Hakikisha unaepuka hamasa ya kuuza nyumba kwa kuipangisha nyumba yako. Ni afadhali kuipangisha nyumba yako kuliko kuiuza kama kweli ulizingatia sababu hizi mbili;-
✓ Usanifu wa nyumba yako ya kuishi (architectural designs).
✓ Eneo nyumba yako ya kuishi ilipo.
Sita.
Mabadiliko ya usanifu wa nyumba.
Kwa kawaida usanifu wa nyumba husika hupoteza mvuto kila baada miaka 20. Hivyo, baada ya miaka 20 toka umiliki nyumba yako ya kuishi inawezekana kabisa nyumba isiwe na mvuto tena.
Kwa lugha nyingine, nyumba yako haitakuwa ya kisasa baada ya miaka 20 ijayo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko makubwa sana ya sayansi na teknolojia.
Hivyo, ni muhimu sana kumiliki nyumba ya kuishi ambayo ina sifa zote za kiuwekezaji.
Saba.
Bahati kwenye safari ya maisha.
Bahati inaweza kuwa mbaya au nzuri. Lakini bahati ni sehemu ya maisha yetu binadamu. Kesho unaweza kupandishwa cheo mpaka kusimamia majukumu ya kitaifa, hivyo hataendelea kuishi kwenye nyumba yako ya awali.
Kesho, unaweza kupelekwa nchi za nje ukatekeleze majukumu ya ubalozi wa nchi yetu. Hivyo, hutaweza kuendelea kuishi kwenye nyumba yako ya awali.
Kesho, unaweza kuchaguliwa kuwa mkuu wa mkoa/wilaya ya mbali na ulipojenga. Hivyo, hutaendelea kuishi kwenye nyumba yako ya awali.
Rafiki yangu, nakushauri usimiliki nyumba ya kuishi ambayo haina sifa za kukuingizia kipato kwa siku zijazo.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Mbobezi wa majengo.
Whatsapp; +255 752 413 711