General mex
Senior Member
- May 1, 2011
- 158
- 185
Ni ukweli usiopingika kwamba sanaa kwa taifa hili sasa imeanza kunufaisha wasanii wengi ambao kazi zao zimetokea kukubalika sana.
Ushauri wangu ni mmoja tuu kwamba, kazi ya sanaa ni kazi nzuri kwa msanii pale ambapo inatokea kazi yake ikapendwa sana ila ni uhakika usiopingika kwamba sanaa hailipi milele, au niseme kwa muda mrefu sana. yaani umri ukisogea na ikatokea aina nyingine ya muziki au filamu na waigizaji wengine wapya, basi unakua umebaki na akiba yako tuu na sio rahisi kutengeneza tena kipato ulichokizoea.
Sasa ili kuhakikisha kwamba maisha hayabadiliki sana hata msanii akifulia, mi nashauri wasanii wote wajifunze kuhusiana na bima za maisha, (annuity, endowment) ambazo zinatolewa na mashirika ya umma au pia kampuni binafsi za bima.
Hapa msanii anaweza akanunua annuity ambayo itakua inamlipa kiasi fulani cha hela kwa muda fulani, hii nadhani itasaidia kuhakikisha kwamba hali ya maisha ya msanii haitabadilika sana hata kama sanaa yake itachuja. mfano mzuri ni msanii wa TAKEU style ambaye alipata hela nyingi sana kwa muda mfupi ila baada ya muda kidogo hakua nayo tena. nawasilisha ushauri wangu kwamba wasanii waangalie sana bidhaa zitolewazo na mashirika ya bima na pensheni nadhani zitawafaa sana.