Ushauri wangu Simba iwaongeze Prince Dube, Manzoki, James Akaminko na Wamerekani wa Singida

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Sisi tunaoifahamu Simba bila ushabiki oya oya tunajua kuwa wachezaji wetu wengi ndani ya Simba hawawezi kutoa ushindani, lazima uongozi, wapenzi, mashabiki na wanachama wakubali kuwa kikosi chetu siyo kipana.

Wachezaji kama Kennedy Wilson Juma, jimmyson Mwinuke, Gadiel Michael, Erasto nyoni, Jonas mkude, Victor Akpan, Nelson Okwa, Peter Banda, Mzamiru, Kanoute, Tshabalala, Kapombe kuumwa umwa, Israel kuumwa umwa, Nassoro Kapama, Mohamed Quattara, John Bocco tayari baadhi yao wameshatumika sana na hawana jipya, wengine walevi na kasi hawana, wengine wazito.

Ushauri wangu, dirisha dogo Simba wavunje kibubu na iwe isiwe iwasajili hawa hapa.

Prince Dube Azam, James Akaminko Azam, Nathaniel, Chilambo Azam, wale Wamarekani watatu wa Singida,
Naftar Nashon Geita, Manzoki na wengineo.


Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Tuna uwezo wa kuvunja mikataba yao???
 
Mkopeshwe kama mlivyokopeshwa Guardiola Mnene😁😁😁😁😊😊😊
 
Hata wakiletwa hao wachezaji wapya bado kocha mzawa ataendelea kutupangia wazawa tu
 
Tukisema mnakikosi kibovu mnabisha
 
Shida ni pesa baba unazani kuna timu haitaki wachezaji wazuri?
 
Simba Ina Mapungufu makubwa sana.

Kama Mo yupo serious anatakiwa aweke Hela nyingi sana , kubwa ya usajili.

Nazani ni zaidi ya Bilioni 2-3 Ili Simba Angalau iwe inafika Nusu Fainali.

+ Proper scatting na sio janja janja.
 
Mo yupi unamzungumzia....Simba hatuna timu mazeee timu ikimkaba chama phiri tumeishaaaa
 
Kwa mpira walio piga leo yanga mwarabu akija taifa anakufa za kutosha tu.
Kama mwarabu atakuja kujidanganya kwamba Yanga sc iliyocheza ndiyo anayokujakukutana nayo kapotezwa. Amini nisemacho.
 
Kwa mpira walio piga leo yanga mwarabu akija taifa anakufa za kutosha tu.
Mpira wa izo penati za kishoga wakishinda Yanga mimi Aziza wa tanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…