Ushauri wangu, ukinunua gari used nenda kabadilishe jina la umiliki

DodomaTZ

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
84
Reaction score
118
Kuna jambo moja ambalo watu wengi huwa ni kama wanachukulia poa lakini kiuhalisia lina maana kubwa, jambo hili ni kubadili jina la umiliki wa gari au chombo chochote cha moto

Nazungumza haya kwa kuwa nimeona mambo kibao yakitokea huko mitaani na menginie ni kwa watu wangu wa karibu.

Unakuta gari imewahi kufanya msala siku za nyuma au mmiliki mwenyewe ana msala, hivyo anapokuuzia kisha ukaendelea kutumia bila kubadilisha jina inamaanisha kuwa lolote likitokea kazi unayo.

Lakini pia hata sheria zinakataza na ndio maana trafiki wakikunasa unatumia gari ambalo lina umiliki usio wa kwako wanaweza kukuchomesha na kukupa msala.
 
Ni hatari sana!!hata Bima,ukikutwa na ajari haitalipa chochote, sema Wa Tz, ni kupenda kupuuzia mambo tu, ila likikukuta, unaanza lawama tena!!
 
Kiusalama Polisi na TRA ndio wadau wako kabla ya kununua gari lolote, polisi kwa ajili ya rekodi za chombo na uhalifu na tra masuala ya kodi, Tatizo letu ni mfumo una gharama zenye urasimu na kupoteza muda. Sasa watu wengi wanaonunua magari used unakuta kapata m10 zake anataka apate gari na abakiwe na chenji ya mafuta na service, ukianza kumwambia mambo TRA anaona ni gharama.

NAPENDEKEZA KUNGEKUWA NA MFUMO WA TRA/TRAFIC VEHICLE CHANGE OF OWNERSHIP PORTAL AMBAO NI ONLINE WANASHERIA WAUTUMIE KWA AJILI YA TRANSFER. UKIENDA KWA MWANASHERIA ANAJAZA FOMU, KISHA SYSTEM INAFANYA ANALYSIS KAMA HAKUNA KODI INAYODAIWA NA HAKUNA CRIMINAL RECORDS SYSTEM INATOA KADI EXTRACT YENYE CONTROL NAMBA YA MALIPO IKILIPWA UNACHUKUA KADI YA ZAMANI, MKATABA NA EXTRACT UNAENDA TRA UNAPEWA KADI MPYA ILI KAMA GARI LINA RECORD ZA MADENI AU UHALIFU PALE PALE WAKATI WA KUJAZA KWA MWANASHERIA ITAJULIKANA NA KAMA GARI IPO SAWA SHUGHULI YOTE INAISHIA KWA MWANASHERIA.
 
logical and practical

TRA wafanyie kazi huu ushauri
 
Kuna jambo moja ambalo watu wengi huwa ni kama wanachukulia poa lakini kiuhalisia lina maana kubwa, jambo hili ni kubadili jina la umiliki wa gari au chombo chochote cha moto

Nazungumza haya kwa kuwa nimeona mambo kibao yakitokea huko mitaani na menginie ni kwa watu wangu wa karibu.

Unakuta gari imewahi kufanya msala siku za nyuma au mmiliki mwenyewe ana msala, hivyo anapokuuzia kisha ukaendelea kutumia bila kubadilisha jina inamaanisha kuwa lolote likitokea kazi unayo.

Lakini pia hata sheria zinakataza na ndio maana trafiki wakikunasa unatumia gari ambalo lina umiliki usio wa kwako wanaweza kukuchomesha na kukupa msala.
Unataka kusema unanunua gari bila mkataba wa mauziano?
 
Ningekua mimi Nina maamuzi ambayo nchi nyingi zinatumia,magari yote yanasajiliwa na metro au municipalities husika, TRA they got nothing to do ,mapato yanayotokana na usajili wa magari na leseni za udereva ni mali ya municipalities husika, gari inapotaka to change hands, mnunuzi kwanza anakwenda traffic dept kupata rekodi ya Ile gari, then police clearance (kama ni stolen vehicle au ilihusika kwenye uhalifu),then mnunuzi unapeleka gari ikafanyiwe roadworthty, haya yakifanyika na kuonekana yapo above the board, then ulipaji unafanyika na unachukua vehicle registration certificate unakwenda nayo municipality kubadilisha ownership, kinyume cha hapo ni utapeli na majanga
 
Msingi wa hoja yako kama sijakosea ni mapato, lakin ukifanya overview ya mfumo mzima wa transfer ni almost the same. Ingawa challenge kubwa sana Tanzania ni wauzaji kutokuwa waaminifu.
 
Kuna jambo moja ambalo watu wengi huwa ni kama wanachukulia poa lakini kiuhalisia lina maana kubwa, jambo hili ni kubadili jina la umiliki wa gari au chombo chochote cha moto

Nazungumza haya kwa kuwa nimeona mambo kibao yakitokea huko mitaani na menginie ni kwa watu wangu wa karibu.

Unakuta gari imewahi kufanya msala siku za nyuma au mmiliki mwenyewe ana msala, hivyo anapokuuzia kisha ukaendelea kutumia bila kubadilisha jina inamaanisha kuwa lolote likitokea kazi unayo.

Lakini pia hata sheria zinakataza na ndio maana trafiki wakikunasa unatumia gari ambalo lina umiliki usio wa kwako wanaweza kukuchomesha na kukupa msala.
Kwa sehemu kubwa upo sahihi, ingawa kutumia gari ambalo wewe siyo mmiliki siyo kosa kisheria hata kidogo as long as halina issues, na pengine zaidi hata ya 50% ya magari huku mabarabarani, yanaendeshwa na wasio wamiliki.
 
Kiusalama Polisi na TRA ndio wadau wako kabla ya kununua gari lolote, polisi kwa ajili ya rekodi za chombo na uhalifu na tra masuala ya kodi, Tatizo letu ni mfumo una gharama zenye urasimu na kupoteza muda. Sasa watu wengi wanaonunua magari used unakuta kapata m10 zake anataka apate gari na abakiwe na chenji ya mafuta na service, ukianza kumwambia mambo TRA anaona ni gharama.

NAPENDEKEZA KUNGEKUWA NA MFUMO WA TRA/TRAFIC VEHICLE CHANGE OF OWNERSHIP PORTAL AMBAO NI ONLINE WANASHERIA WAUTUMIE KWA AJILI YA TRANSFER. UKIENDA KWA MWANASHERIA ANAJAZA FOMU, KISHA SYSTEM INAFANYA ANALYSIS KAMA HAKUNA KODI INAYODAIWA NA HAKUNA CRIMINAL RECORDS SYSTEM INATOA KADI EXTRACT YENYE CONTROL NAMBA YA MALIPO IKILIPWA UNACHUKUA KADI YA ZAMANI, MKATABA NA EXTRACT UNAENDA TRA UNAPEWA KADI MPYA ILI KAMA GARI LINA RECORD ZA MADENI AU UHALIFU PALE PALE WAKATI WA KUJAZA KWA MWANASHERIA ITAJULIKANA NA KAMA GARI IPO SAWA SHUGHULI YOTE INAISHIA KWA MWANASHERIA.
Hii proposal yako na yenyewe ina downside yake, kuna mtu unakuta ana card mbili za gari, ndo maana kwendana na hizi challenges, moja ya requirement TRA waliyokuja nayo ni kwamba, wakati wa transfer gari physically liwepo ingawa wengine wanapuuzia hii procedure ingawa inalenga kumlinda mteja asidhulumiwe.

*Usikubali kulipia gari kwa kupewa card original kwa miadi ya kwenda kuchukua gari kesho, ni hatari sana.
 
Kubadirisha gharama.
Gharama za kukamilisha transfer kisheria kila mtu ana part yake (aliyeuza na aliyeuziwa), wote mnatakiwa kuchangiana ingawa siyo kubwa, na kwenye gharama mnunuaji hulipia gharama ndogo zaidi kuliko muuzaji (but it depends).

Ukiangalia transfer costs vs risks, cost ya transfer ni ndogo kuliko associated risks.
 
Msingi wa hoja yako kama sijakosea ni mapato, lakin ukifanya overview ya mfumo mzima wa transfer ni almost the same. Ingawa challenge kubwa sana Tanzania ni wauzaji kutokuwa waaminifu.
Agreed mkuu ila ni muhimi kufuata utaratibu uliopo, mkuu why ununue gari bila ya kujiridhia kama gari ni halali na nzima?,gari sio chapati ya just to exchange money!,wengine humu wanauziwa mpaka nyumba bila documents au kujiridhisha it's craze mkuu
 
Correct. Kwa mazingira ya Tanzania, ni very extremely dangerous & reckless. Binafsi siwezi kukubali ku-accept hiyo risk.
 
Swali langu kama ulinunua gari lakini aliyekuuzia nayeye aliuziwa na hakubadili umiliki.hapo process inakuaje wakuu? Na vp kama hana access na yule mmiliki wa mwanzo?
 
Back
Top Bottom