ushauri wangu wa kufungia mwaka kwa diamond platnumz

kijanamtanashati

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2014
Posts
516
Reaction score
905
Ukizungumzia DIAMOND PLATNUMZ bila ya ubishi wala kupinga basi unakuwa unazungumzia msanii mkubwa barani afrika na duniani kwa ujumla. Msanii ambae ameweza kukaa kileleni tangu anatoka mpaka hivi sasa. Msanii anaejituma kila kukicha na jitihada zake zinaonekana kila uchwao.

Diamond ni msanii wa muziki mmoja wapo kati ya wachache waliopo duniani ambao wana uwezo wa kucheza na kudance vizuri sana. Lakini ukiangalia video za nyimbo zake na zile za behind the scenes basi utagundua huyu kijana ana uwezo mkubwa sana wa kuigiza. Kutokana na hiki kipaji chake cha kuigiza alicho nacho namshauri asikiache kiende hivi hivi au kiishie kwenye video za nyimbo zake tu. Ajaribu kutoa movie angalau moja na yeye ndo awe leading character.

Kwenye suala la scenario hilo haina shaka kwasababu nina uhakika huwezi kukosa scenario kali ya kufa mtu(sio kama za wabongo muvi za hadithi hadithi njoo utam kolea). Kuhusu waigizaji haina haja ya kuwaweka hawa wauza sura wasiokuwa na vipaji ambao tumezoea kuwaona wakiuza sura kwenye muvi. Kuna waigizaji chipukizi kibao ambao wana uwezo mkubwa wa kuigiza kuliko hawa tulio wazoea.

Tukija kwenye suala la biashara na matangazo hapa sihitaji kukushauri maana nina uhakika wa 100% wewe ni mfanya biashara mzuri sana. Hivyo muvi ambayo utaitoa naamini una uwezo wa kuisimamia vizuri katika mauzo kama vile wanavyofanya wenzetu wa Europe na sehemu nyingine zilizoendelea, yani kutoa muvi na kuipeleka kila mkoa na watu wawe wanaangalia kwenye nyumba maalum za kuoneshea sinema kama vile mlimani city(najua Tanzania sio kila mkoa una sehemu ya kuoneshea cinema kama ilivyo mlimani city lakini unaweza kuanza na mikoa ambayo ina uwezo huo). Baadae sana kama mwezi mmoja au miwili unatoa CD ili kuwafikia wale ambao hawakuweza kuona muvi hiyo ukumbini. Kwa ushawishi ulio nao kwa sasa nathubutu kusema utauza sana sio kwa Tanzania tu, hata nje ya Tanzania. Diamond uchukue huu ushauri usiupotezee!!

kijanamtanashati
 
Kakusikia mkuu nadhani changamoto itakuwa latiba maana muvi sio kitu cha mchezo mchezo huwa alazi damu anapoona fulsa uyu dogo tumpe mda tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…