AZUSA STREET
JF-Expert Member
- Oct 31, 2013
- 2,007
- 1,897
nilikuwa sijaelewa, nyie wenzetu milioko maeneo ya magereza ambayo wale watuhumiwa wa ugaidi wanaoshitakiwa pale kisutu dsm, na wale waliosomewa leo arusha, je? wamewekwa mahabusu moja?nina maan awapo chumba kimoja? hatari ninayoiona ni kwamba, wakiwekwa pamoja kule gerezani wanaweza kuwa wamepewa uwanja mzuri sana wa kujadili na kupanga namna ya kuendeleza ugaidi wakiwa ndani na nje, ili wavurugane kabisa na wasiweze kabisa kuwasiliana (kwasababu hawana dhamana), wanatakiwa watenganishwe waonene tu siku ya kesi kutajwa ila wakiwa kule gerezani wawekwe maeneo maalumu yenye ulinzi na watenganishwe kabisa na kuwe na inteligensia kule gerezani kuona wanawafundisha nini wafungwa/mahabusu wengine.
naomba magereza ya arusha na dsm mfanye hili kama hamjafanya, mkiwaweka pamoja ni sawa na mmewapa nafasi ya kukaa kikao wao na kujadili namna ya kuiharibu zaidi hii tz ambayo tulizoea kuishi kwa amani. Mungu ibariki tanzania.