Ushauri: Waziri Jafo chukua hii kupunguza uharibifu wa mazingira katika majiji yetu

Nawatania

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
148
Reaction score
549
Kwanza naomba niipongeze Serikali kwa ujenzi wa miundombinu katika majiji yetu ni jambo zuri kuonyesha kodi zetu zinatumika ipasavyo, Dar es Salaam na majiji mengine imekuwepo miradi mikubwa na midogo ya ujenzi wa barabara mfano mwendokasi Dar es Salaam.

Lakini miradi hii imekuwa ikiacha uharibifu kukubwa wa mazingira na kuongeza joto maradufu kwenye majiji yetu, Angalia zilipopita barabara za mwendokasi pote maua miti imekuwa ikikatwa na hakuna miti mipya inayopandwa.

Ushahidi ni Kimara- Kivukoni/ Moroco miradi hii ulikata miti mingi na kuharibu Maua mengi bila kupanda miti mipya na bustani mpya pembezoni mwa barabara.

Sasahivi kuna mradi wa kutoka Kariakoo kwenda Mbagala ukiangalia uharibifu unaofanyika juu ya mazingira ni mkubwa na hakuna jitihada zozote za kupanda miti na maua pembezoni mwa barabara ili kunusuru uharibifu huu.

USHAURI

Joto linaongezeka kwa kasi Dar es Salaam na majiji mengine sio kwa bahati mbaya au kwa sababu ya uwepo wa Bahari pekee bali pia ni kwa sababu ya ukataji miti na uharibifu wa bustani bila kupanda mingine.

Ramani za ujenzi wa Magorofa hazionyeshe sehemu za project za bustani na miti hasa katikati ya miji hii sio haki hata kidogo kwa uhai wetu miaka inayokuja hewa ya Oksijeni itakosekana kabisa.

Hivyo nashauri wangu miradi yote ya ujenzi kuanza barabara, Magorofa, Nyumba za kawaida na miradi mingine izingatie upandaji wa miti pembezoni mwa miradi hiyo pia waboreshe bustani katika miradi yao.

Wizara itunge sheria na ipitishwe na bunge kwamba kila Mtanzania anatakiwa kupanda mti tarehe moja mwezi wa kwanza kila mwaka pia kila Nyumba inayojengwa lazima itenge sehemu za kupanda maua au bustani zingine ili kuboresha mazingira.

Tuchukue mfano wa Dar es salaam labda tuseme ina watu milioni 6 kila mtu apande mti mmoja kila mwaka maana yake tutakuwa na miti mingi badae na itatusaidia kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa nchini.

Tusipochukua hatua miaka 5 ijayo Dar es salaam itakuwa na joto kali sana kama baadhi ya miji ya uchina.

Picha ya kwanza ni Ubungo interchange na picha ya pili ni Nairobi Thika Highway angalia mpangilio wa ujenzi wa barabara na Bustani.

images (8).jpg
images (14).jpg
 
View attachment 1854495View attachment 1854496

Waziri Jafo naomba ichunguze hii kampuni kweye picha hapa chini, inafanya nini? Naona uharibifu mkubwa wa mazingira unafanywa na kampuni hii. Watu wa mazingira wanafanya nini Waziri Jafo?

1641244247655.png
 
Back
Top Bottom