SoC01 Ushauri/wazo muhimu kwa Wizara ya Maliasili na Utalii

SoC01 Ushauri/wazo muhimu kwa Wizara ya Maliasili na Utalii

Stories of Change - 2021 Competition

Mwalimu wa Zamu Tz

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2021
Posts
1,053
Reaction score
2,757
Habari wanajamvi

Tuendelee kuchukua tahadhari juu ya janga hili la CORONA.

Basi bila kupoteza muda nielekee moja kwa moja kwenye lengo la Uzi..Wakuu baada ya mawazo yangu kusikilizwa na waziri wa teknolojia DKT.Faustine Ndugulile na kufanyiwa kazi ipasavyo najihis ni mwenye Furaha sana kama nilivyoeleza kwenye Uzi wangu


uliopita...Sasa nimekaa nikapata wazo jingine ambalo kwasasa linamfaa/linafaa kuwasilishwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt kt. Damas Daniel Ndumbaro

Screenshot_20210823-012123.jpg

Sasa wakuu katika sekta ya Utalii hakuna kitu muhimu kama Branding...bahati mbaya sana Waziri wote wanaopewa wadhifa wanaacha sana ichi kipengele cha Branding...Nyie wenyewe ni mashahidi mnaona jirani(Rwanda) vile wanafocus kwenye kubrand nchi yao kwaivo wameingia parternaship na team kubwa duniani kama Arsenal na sasa PSG..na matunda wanayapata kwasasa sidhani kama kuna nchi Africa mashariki na kati inayoizi Rwanda kwa Utalii achilia mbali kudhorota kwa sekta iyo kwa mwaka 2019/2020 kutokana na janga ili la CORONA lakini ndugu zetu Rwanda bado wanapata wageni wengi kutoka nchi mbalinbali hii inaonesha namna gani branding inaweza kuleta Tija katika sekta

2893579_Screenshot_20210823-012406.jpg
hiyo...Aidha,Waziri wa utalii aliepita Mh. H.kigwangala juzi ametoa ufafanuzi kwamba nayeye wakati anawadhifa huo alikuwa na plan ya kutangaza utalii kupitia team zinazocheza EPL lakini kutokana na sababu kadha wa kadha hakuweza kufanikiwa katika jambo ilo..na anasikitika mpaka sasa bado anamajuto ya kutokamilisha suala ilo..Tunaweza kujibrand kwa njia nyingi tofautitofauti

Screenshot_20210823-022725.jpg

Lakini ukiachana na hoja ya Mh.H.kigwangala. Mimi naona sio lazima tuige Nasisi tuwekwe kwenye team eti (Visit Tanzania au Visit kilimanjaro) Hapana katika jezi zile za Simba za CAF naona inatosha kabisa ila sasa tuangalie namna nyingine ya kujibrand..Na hapa ndio nikawa nawazo la kuwasilisha kwa Waziri wa Utalii ya kwamba anaweza kuingia partnership na MICROSOFT (moja ya kampuni bora duniani) ambao utatuwezesha nasisi kutangaza vivutio vyetu kupitia WINDOWS PC's,,TABLETs n.k n.k kama ambavyo baadhi ya nchi kama S.Africa wanafanya.

images (3).jpeg

Iko ivi ukiwa na PC/Tablet/Desktop ya kuanzia latest window 10 pale unapoiwasha itakuletea ile lock wallpaper sasa ile Lock wallpaper zaman walikua wanaleta logo za window lakini kwa sasa wanaleta picha(HD kabisa) ya vivutio mbalimbali duniani....mfano mimi nilipo Update window yangu ikawa Latest version ya Window 10 pro nikawasha mara ya kwanza ikaleta lock screen ya CAPE TOWN ya S.Afruca aaafu kuna vimaneno pale vinauliza (Je umeipenda hii sehemu na unatamani ufike siku moja? Kama umeipenda tufollow katika page zetu za instagram kupata detail kamili kuhusu sehemu hii" in English lakini)sasa ukifollow iyo page unakuta ni page ya utalii ya S.Africa na apo utapata detail zote ikiwemo maradhi,makazi,hali ya hewa n.k Kiukweli zile Landscape za Cape town zinavutia sana wakati mimi najisemea siku nikipata pesa lazima niende..Nauhakika kuna wenzangu uko duniani wanasema apa kazini wakinipa kashort holiday tu Lazima niende Cape town kushuhudia izi Landscape....

JE TANZANIA TUNASHINDWA ATA BRANDING YA NAMNA HII?? Kwa ufupi tu tunaomba kusummarize mambo..Ni kwamba..Tunatoa ushauri kwa Waziri wa sekta ya Utalii aingie makubaliano na MICROSOFT kupitia WINDOW ili aweze kutangaza vivutio vya Utalii vya nchi yetu kupitia Wallpaper zitakazooneshwa kwa watumiaji wa VIFAA VYA WINDOWS Kote duniani pia anaweza kuongeza ubunifu sio lazima kuingia partnership na MICROSOFT anaweza kuingia ata na TECNO za wachina na watatangaza vivutio vyetu kupitia Wallpaper ....

GOOGLE pia kwa watumiaji wa PC kuna button ya customization ambapo inamruhusu mtumiaji kuchagua wallpaper abayoipenda.
JE hata hii INATUSHINDWA WAKUU???
[

FOCUS ON BRANDING

#Nawasilisha
#storyofchange
#vote
#Support
#AHSANTE..

Screenshot_20210823-012406.jpg
 
Upvote 3
sahihi kabisa hata mim huwa naclick pale kupata maelezo ya picha husika.
tuna maeneo yanye fukwe mfano kigambn ulipaswa uwe tour destination nzuri kwa beaches zake
 
sahihi kabisa hata mim huwa naclick pale kupata maelezo ya picha husika.
tuna maeneo yanye fukwe mfano kigambn ulipaswa uwe tour destination nzuri kwa beaches zake
Ndio mkuu....wizara ifanye kitu viwekwe na vivutio vya TZ pale
 
Back
Top Bottom