Habar za humu ndan members naomben ushaur na msaada wenu jinsi yakutumia calender. Ili kuzunisipate mimba na kujua mzunguko wangu ni mrefu or mfup or wakawaida
Kuanza mwenz wa kumi na moja siku zangu niliziona tarehe 24-27 mwenz wa kumi na mbil siku zangu zili anza tarehe 25-28, mwenz wa kwanza tarehe 20-23 .msada wenu jaman naomben
Anza kuzihesabu toka siku ya kwanza ya MP moja hadi siku moja kabla ya MP nyingine. Huo ndo mzunguko mzima wa hedhi.
Kwa tarehe ulizoweka, mwezi wako mrefu ni siku 31 na mfupi ni siku 26. Lakini, unapaswa kurekodi mizunguko walau 6 kuwa na uhakika wa mwezi mrefu na mfupi.
Kujua siku za hatari, chukua mwezi wako mfupi toa siku 18 na mwezi wako mrefu toa siku 10.
26 - 18 = 8
31 - 10 = 21
Maana yake, siku ya 8 ya mzunguko wako wowote hadi ya 21 ni za hatari. Hivyo usifanye kabisa km hutaki ujauzito, au jikinge. Siku nje ya hizo, jiachie kwa raha zako.
Narudia, rekodi kwa umakini mizunguko yako kwa walau miezi 6 ndipo utapata uhakika wa mwezi mrefu na mfupi. Bila hivyo, hesabu hiyo hapo juu inaweza kukosea siku moja ikala kwako.
Sijui kwanini zinatumika siku 18 na 10!
Kwa hisani ya aliveprojects.com
sawa kabisa mkuu... ila kwa tahadhari wote wenye mzunguko mfupi njia hii siyo rafiki sana kwao.
Siku kubadirika badirika inasababishwa na mengi wala isikutishe saana
Labda Mazingira tofauti ya hali ya hewa,au kama uliwahi kutoa ujauzito, msongo wa mawazo na vyakula!
Hizo ni moja ya sababu za mzunguko kubadirika badirika
Ila yote kwa yote ili usikosee kalenda kama huwezi kuzi mantain tarehe za hatari basi
tumia condom mara kwa mara
Mwambie mmeo/mpenzio awe anamwaga nje kabla ya kufika kileleni
na hizo ni some scientific method ukitaka zaidi hasa kujua tarehe vizuri nimeku pm namba hapa sikai online saana!