Ushauri wenu jamani

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
Mimi nataka kujua tu namna ya kumuacha mume wangu. Iko hivi, nimeolewa, ndoa yangu ina miaka 12, lakini katika kipinipidi chote hicho sijawahi kufurahia maisha ya ndoa, kila siku mimi nniwakulia na wanangu, tunagombana kiasi kwamba sasa hivi hata tendo la ndoa hakuna.

Si kama ananip*iga wala kunitukana, hapana, mume wangu anahudumia familia, anajali, anatoa kila kitu, huwezi kumuomba akakunyima, anafanya kazi na mimi kanifungulia biashara mara 4, lakini ilishindikana kwa sababu sikuwa na amani ya roho. Shida, mume wangu ni mtu wa kazi, hana muda na familia, yaani hana yale mahaba, huwezi amini mume wangu hajawahi kuninunulia zawadi yoyote, hajawahi, ukimuambia anakwambia hela si zipo, wewe nenda mimi ninunue. Yaani kuliko kuninunulia kitu anakupa hela!

Unaweza kusuka, anakupa hela, lakini hata kukusifia umependeza hatusifii, yaani ni majirani na watu wa nje. Rafiki zangu wakija nyumbani waninisifia, lakini yeye hata hajali na hanioneshi wivu kabisa.

Naweza kumuaga naenda nyumbani kwa mama, nikaenda hata wiki lakini hajali, hawezi kufuatilia kama nimeenda kweli au niko kwa mwanaume.

Baada ya kuona hivyo, niliamua kuchepuka makusudi ili aone wivu, ila haonyeshi tofauti, nimejaribu kumuonyesha vituko ila hajali, mpaka kuna wakati natamani kujirekodi nikiwa na mwanaume mwingine nimtumie, ila naogopa itakuwa aibu kwa ndugu zangu.

Kuna kaka niko naye, yeye ni mdogo, mimi nina miaka 42, yeye ana miaka 31, amemaliza chuo lakini hajapata kazi, niko naye kwenye mahusiano huu ni mwezi wa 6, nina furaha sana, na ananipenda, yaani mwanamke ujajaliwa mpaka unajiona malaiika, asubuhi anakutumia emoj nyingi za mapenzi, mchana ndiyo, atataka kuja, kila wakati ana muda na mimi sana.

Mimi sina kazi, na yeye hana kazi, lakini mimi na mume wangu tumejenga, tuna nyumba tano, mbili zina majina yangu na tatu zina majina yake, ambapo moja ndiyo tunaishi. Hizi zangu ni za kupangisha, na kodi nachukua mimi, mume wangu haniulizii.

Sasa ninachouliza, je, nikaachana na mume wangu, kwani tutagawana na hizi nyumba zangu? Mimi sijali kuhusu zake, kwani zangu ziko sehemu nzuri, ni yeye alijenga bila kundiandika mimi. Nataka talaka, lakini nataka kila mmoja abaki na nyumba zake, kwani mimi na huyu mwanaume niliye naye tumepanga kutengeneza BNB kwenye hizi nyumba zangu, tuwe tunasimamia wote, nataka tu mume wangu asizidai!
 
Ulipojaribu kuchepuka tu ndyo umeharibu sasa huko ulipochepukia umepata ulichotaka wanawake kama nyinyi wachepukaji msiojeshimu ingekua enzi zangu zile nakuchimbia shimo nakuzika hai
 
Unachokitafuta utakipata endelea utakuja kujuuta
 
KWELI mkataa pema pabaya panamwita
 
Duh, Wakuu wanakushauri urudi Facebook, kwakuwa hapa ni jukwaa la great thinkers. Kama unakubaliana na ushauri wao, basi nenda na andiko hili: Waefeso 5:3-4
"Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu. Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai..."
 
Your browser is not able to display this video.
 
namna ya kumuacha mume wangu
Samahani unajinsia gani?? Hapa ulisema hivi:

Hii kweli nimeshuhudia aisee kuna mmoja ananilalamikia hata wa kuzaa nae aisee






 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…