Ushauri wenu, kushiriki kwa mwenza wa kike katika suala la biashara

Ushauri wenu, kushiriki kwa mwenza wa kike katika suala la biashara

2v1

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2024
Posts
247
Reaction score
358
Wanandoa na mliowahi kuishi na wanawake naombeni ushauri kidogo, huwa napenda sana kujifunza mawili matatu kabla, ili niweze kufahamu walau kwa uchache jambo ambalo nakwenda kulifanya, wenda isiwe mipango ya sasa lakini najua nitalifanya.

Binafsi ndiyo najitafuta kimaisha, napenda sana biashara nadhani ndiyo kitu ambacho naweza nikawekeza sana sehemu hiyo. Natamani siku moja niwe na mwenza sahihi, kuna muda huwa natafakari kuhusu hawa viumbe kuna muda huwa kama siwaelewi hivi.

Swali:
Nitakapokuwa na mwenza nimshirikishe kwenye biashara au niwe nazipambania mwenyewe au awe na kazi yake tu au awe ajua kwa juu juu tu au awe mama wa nyumbani tu maana huwa nafikiria ikitokea nimeenda mbali kibiashara au kuumwa kwa muda kidogo.

Je, ni nani atakaye zisimamia biashara hizo?
 
Watu wanatofautiana ila binafsi mke niliyenaye nilibaini yafuatayo baada ya kumshirikisha kwenye biashara:
1. Alipoifahamu vizuri biashara alitaka kujimilikisha iwe yake binafsi na sio yetu sote
2. Alianza kuchukua fedha bila kunitaarifu na kujiunga kwenye vikundi vya kupeana
3. Nilipokuwa namueleza kuhusu kuepuka matumizi yasiyo muhimu aliona namnyanyasa.
Mambo ni mengi Ila mwisho wa siku niliamua kumwachia biashara na haikuchukua muda akafirisi
 
Kama ni mke wako ni vyema ukamfundisha, mkawa mnapambana wote ni kitu kizuri, hata Mungu atatia baraka.

ila kama ni mchepuko usiwahi kujaribu hicho kitu, Pambana pekeako
 
  • Thanks
Reactions: 2v1
Watu wanatofautiana ila binafsi mke niliyenaye nilibaini yafuatayo baada ya kumshirikisha kwenye biashara:
1. Alipoifahamu vizuri biashara alitaka kujimilikisha iwe yake binafsi na sio yetu sote
2. Alianza kuchukua fedha bila kunitaarifu na kujiunga kwenye vikundi vya kupeana
3. Nilipokuwa namueleza kuhusu kuepuka matumizi yasiyo muhimu aliona namnyanyasa.
Mambo ni mengi Ila mwisho wa siku niliamua kumwachia biashara na haikuchukua muda akafirisi
Huu ushauri huu utaukumbuka baadaye note hii point kubwa sana
 
Biashara unafungua wewe ili iwasaidie wewe, yeye na familia Mwisho wa siku inakuwa yake, unaamua kumuachia aiendeshe walau imsaidie ghafla inageuka dhamana ya mikopo kausha Damu, Mikopo Umiza mwisho wa Siku dhahama ya Malejesho unaludishiwa wewe, Sio wote ila Dah hawa watu sijui wanawazaga nini?
 
  • Thanks
Reactions: 2v1
Kila mtu awe na biashara yake.

Ku-share biashara na Wanawake wa kiafrika ambo wengi wao UPEO mdogo ni kujitafutia matatizo
Naona imeka poa kiasi pia naona kama akiwa na roho ya ubinafsi kidogo itakuwa shida, maana unaweza ukakuta swala la kusaidia familia yake kwa upande wake likawa poa ila ikaja upande wako kukawa shida kidogo, kuna muda mambo huwa yanayumba ukakuta biashara zimeshuka ghafla. Ingawa uwezi kumpata aliye kamilika kwa kila kitu
 
Back
Top Bottom