ushauri wenu Muhimu;Mtoto kaota jino moja tu...

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2010
Posts
1,945
Reaction score
728
Habari wakuu! Nina mtoto wa miezi 11 ana afya nzuri tu lkn alichelewa kuota meno ila yalipoanza kuota ya chini nimeshangaa ameota jino moja kwa upande wa chini na ya juu yanatokea yote mawili.
Naomba ushauri kwa wanaojua je hii inaweza kusababishwa na nini maana jino moja la chini lilioota lina kama 1.2mm wakati hakuna dalili ya kuota jino la pili.
 
pia unaweza kuomba ushauri zaidi kwa dentist ili akutoe wasiwasi ulionao. hakuna mtu anayekosa meno ila huchelewa tu kidogo
 
Husiwe na wasiwasi yataota tu..Mwanangu yalianza meno ya juu yakafika manne wakati chini hakuna kitu, sikuwa na wasiwasi kwani ninajua binadamu tunatofautiana.. na baada ya muda likatokea jino moja chini, after kama 2months likatokeza la pili yake.. Ni kawaida sana. (Kama ingekuwa enzi zile basi mbona nisingekuwa na mtoto si unajua zamani ilikuwa kama mtoto anaanza na meno ya juu basi ni mkosi)
 

Asante kwa ku share uzoefu wako mkuu! unajua binafsi sijawahi kukutana na hali hii japo hako ni ka 2nd born
NAKUSHUKURU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…