Salam wakuu wa kazi. Mimi mwenzenu nataka sana kuwa mjuzi wa kuandika research. Nilipata kumuona jamaa mmoja alikuwa f4 leaver akawa anafanya kazi za kujitolea na taasisi za utafiti lengo ikiwa ni kupata uzoefu na utaalam wa kuandika research. Leo jamaa ni hatari anafanya na kuandaa vizuri sana research. Hivyo alinihamasisha sana. Maana nilipata kusikia hii ni kitu muhimu sana kwenye kozi yoyote chuo na ni tatizo kwa wanavyuo wengi kumaliza bila kujua kuaandaa vyema tafiti. Naomba msaada wenu kwa anayejua naweza kupata wapi hizo taasisi hapa Dar. Mimi nasoma elimu ya watu wazima. Shukrani!