Ushauri wenu ni muhimu sana na nauhitaji mno katika hii azma yangu ya kutaka Kujiajiri kuliko Kuajiriwa Tanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nafikiria kuanza kuwa nazungukia Ofisi za Taasisi mbalimbali nchini Tanzania hasa zile zenye ' Mabosi ' wakubwa wakubwa ( CEO's ) na ikibidi hata na Viongozi wa Serikali na Kitaifa ili niwe nawasaidia ' Kuwatunzia ' Mafaili yao mengi ambayo mengine huwa wanayaweka hadi Vitandani yakisubiriwa Kusainiwa.

Nitakachokifanya tu ni kwamba Mimi nitakuwa nayaendea huko huko hayo ' Mafaili ' na kuyachukua kuja kuyahifadhi Kwangu, kisha nayapanga vizuri na asubuhi hao ' Mabosi ' na ' Viongozi ' wakishaamka tu nawapelekea ili Kazi yao ya ' Kusaini ' ianze kuliko kulala nayo hapo hapo Kitandani halafu bahati mbaya labda waje ' wayakojolee ' au wayadondoshee ' Maudenda ' bure.

Na gharama yangu ya Kuyahifadhi hayo ' Mafaili ' itakuwa ni ndogo sana na nitayatunza vyema kabisa hadi wenyewe watafurahi. Lengo langu Kuu hapa ni kuwapa hao ' Mabosi ' na ' Viongozi ' muda mzuri wa Kupumzika na Wake zao kuliko muda mwingi hata usiku wa manane wao Kuwaza ' Kusaini ' tu ' Mafaili ' tena wakati mwingine wakiwa wamechoka au wana ' Stress ' zao nyingi halafu wakajikuta wanaharibu kila kitu.

Nitawashukuruni kama mtanishauri vyema katika hili wana JamiiForums wote ili nami GENTAMYCINE niweze sasa Kujiajiri au kuwa Mjasiriamali wa Kutunza ' Mafaili ' yanayotunzwa Vyumbani ama yasikojolewe au yasidondokewe hovyo na ' Maudenda ' yanayotokana na Mtu Kushikwa na Usungizi mzito.

Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…