Ushauri wenu wadau. Nimefungua kesi ya kutapeliwa na foreigner wa Uswis na amerudi kwao kaacha mke n

Rally

New Member
Joined
Feb 20, 2015
Posts
1
Reaction score
0
Jamaa aliniuzia pikipiki kwa ml3.7 kwa awamu 2 ndani ya mwezi mmoja.
Ya kwanza tar14 Sept nilimpa ml2.4 tukaandikiana shahidi wake ni mke wake(ni Mbongo). Malipo ya kwanza tulikubaliana nichukue copy za nyaraka za pkpk.
Tar14oct nikaenda nyumbani kwake kumalizia malipo nayeye anikabidhi pikipiki na nyaraka zote halisi.
Nikakuta ameweka bond pkpk na riba imezidi kiwango anachonidai hivyo hawezi kuikomboa, akaniambia atanilipa mwisho wa mwezi wa oct.
Mwisho wa mwezi nikasafiri akanipigia simu amepata m1 then atanimalizia iliyobaki baada ya mwezi, bahati mbaya sikufanikiwa kurudi mapema.
Niliporudi mjini nikaenda nyumba aliyokuwa anaishi, jirani yake akaniambia amesafiri na mkewe amehama.

NIMEFUNGUA KESI POLISI WAMENIAMBIA NIMTAFUTE/ NIMSUBIRI HADI ARUDI.

Nafahamu anapoishi mama wa mke wake.

Je naweza kumshtaki kupitia ubalozi wa nchi yake?
Wapi pa kuanzia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…