Ushauri wenu wadau

Ushauri wenu wadau

mtima nyongo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
1,947
Reaction score
2,047
Gari yangu ni gx100 cresta cc2000 tatizo la hii gari ni nguvu,
Kupanda milima aina nguvu kabisa na niliipeleka service na fundi akaikagua engine na kuniambia hii gari ili iwe sawa inabidi kushusha na kuichambua engine ili kila kibovu kitupwe na kuwekwa kipya au nitafute engine nyingine maana hata nikirekebisha hii muda si mrefu itasumbua tena.
Sasa wakuu hapo mnashaulije niirekebishe hii hii au ninunue engine nyingine na ghrama ya engine nyingine itanigharimu kiasi gan?
Naombeni ushauri wenu wadau
 
Ngoja wanao miliki magari waamke aiseee....
[emoji605] [emoji605] [emoji605] [emoji605] [emoji605]
 
Ngoja wanao miliki magari waamke aiseee....
[emoji605] [emoji605] [emoji605] [emoji605] [emoji605]
Jibu lako ni sahihi kanisa ila isije wakakuna una mtima nyongo kwa kuwa wewe wamiliki baiskeli
 
Cha msingi ni kutafuta fundi mzuri wa overhaul ya injini maana zile injini nyingine zinauzwa ni kama yako tu imepigwa service ya kueleweka inawekwa sokoni
 
mkuu hapo kuna mambo mawili.kwanza kuna engine na gearbox .na hapo ndio ufundi unatakiwa na ili uwe fundi mzuri ya kupasa uwe unaweza kutambua matatizo na sio kulekebisha tatizo?? kujua tatizo ndio ufundi.

labda nikuulize maswali machache kwani paformance ya engine ikoje??

je huko kukosa nguvu unauhakika ni engine na sio gearbox??

je ukiwa unapanda mlimani na gari unaposema kuwa inakosa nguvu revolution/rpm huwa inakuwa kwenye ngapi?? mfano unapokuwa speed 20 or 40 rpm huwa inakuwa kwenye ngapi??

usije ukanunua engine na tatizo likawa gearbox au ukanunua engine kumbe tatizo ni sensor 1 tuu kwenye engine??

na kama ni engine kukosa nguvu vitu ambavyo vinaweza kukufanya ununue engine labda kuwe na ubovu kwenye block au cyrinder head au kama mashine inataka kufanyiwa ovarhall hapo sawa.

mkuu upo mkoa gani
 
Cha msingi ni kutafuta fundi mzuri wa overhaul ya injini maana zile injini nyingine zinauzwa ni kama yako tu imepigwa service ya kueleweka inawekwa sokoni
Asante mkuu kwa ushauri na ntaufanyia kazi
 
Back
Top Bottom