Habari za kazi wana JF. Naomba tusaidiane kumshauri huyu dada yetu.
Kuna dada nafahamiana naye vizuri yupo Dar na ana mtoto mmoja alizaa na bwana miaka kumi iliyopita. sasa nanasema amepata bwana wa kikongo ambaye amehamia kwake na wanaishi pamoja ila huyo bwana kipato chake kidogo na yeye dada mambo yake siyo mabaya kwakweli. Ila kwa ufupi huyo bwana alikuwa na watoto watatu huko kwao sasa anataka awalete watoto wake hapo kwa huyo dada. Wasiwasi wa dada ni je huyu jamaa anampenda kweli au anataka kumletetee mizigo tu kwani jamaa hajawa stable na maisha yake bado.
Kabla hujampa ushauri kwanza muulize,
1.Yeye huyo dada mwanae wa miaka 10 yupo wapi? wataishi nae?
2.Mkongo wameishi nae kwa muda gani?
3.Mama wa hao watoto 3 yuko wapi? bado ni mkewe au la?
4.Mama wa hao watoto akiamua kuja waona wanawe Dar yupo tayari kuishi nae?
5.Ndugu/wazazi zake huyo mama na ndugu/wazazi wa mcongo wanajua huo uhusiano?
Majibu ya hayo maswali yatakupa mwanga zaidi wa nini cha kufanya.
Kwa kawaida binadamu huzua jambo,jambo likawa tatizo, mwisho likawa tatizo kubwa kabisa likamzidi na kumshinda.
HE, UNAULIZA KAMA ANAKUPENDA? akupendae ni yule anaekupa raha zote,anakujali na kukutunza hakuongezei matatizo ila hupunguza matatizo yako kama si kuyamaliza.(huyu mcongo anaongeza matatizo ya watoto 3 au anapunguza?)
Hata kama kazi yake ya salon au muziki sijui, ikichanganya, sidhani kama anafaa.