SoC01 Ushauri: Zingatia mambo haya utafanikiwa haraka

Stories of Change - 2021 Competition

Marjo Mlekwa

Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
38
Reaction score
60
Nadhani makala hii haitawahusu vijana wavivu ambao wao wanawaza kuamka nakukaa vijiweni wakipeana mbinu za kupora nakuiba mali za watu.

Hii itawahusu vijana na watu wazima ambao bado wangali kwenye mapambano yakujikwamua nakufikia bango lenye nembo ya mafanikio.

2852601_IMG-20210722-WA0011.jpg

Zipo siri nyingi sana zenye uwezo wakukuvusha daraja kutoka mahali ulipo nakuyafikia mafanikio unayoyaota, nakuyatamani,kila siku watu wanazungumzia kufanya kazi kwa bidii, juhudi na kijituma kuwa ndio nyenzo zakumfanya mtu afanikiwe.

Nakubaliana nazo nyenzo hizo na nyengine nyingi zinazozungumzwa na watu wengi lakini mimi leo nitaongelea tatu tu...

Ya kwanza ni njia ambayo kitaalamu utaitamka kama The Past Is Gone ila mimi nitaiandika kwa kiswahili fasaha kabisa nikiitaja kama YALIYOPITA SI NDWELE, nyingine ni umuhimu wakusema neno HAPANA na njia ya tatu tutaitazama NGUVU YAKUTOA

1: YALIYOPITA SI NDWELE.

Ni wengi niliozungumza nao kuwapima misimamo yao ya kimaisha walitamka kuhusu makosa ya wazazi wao kuwagharimu katika kutimiza malengo yao...

"baba angenisomesha ningekuwa nimefika mahali fulani"

Wengi husema hivi au wengine hulaumu uzembe wa makosa yao waliyoyafanya shuleni wakiamini kuwa ndio chanzo cha wao kushindwa kutimiza malengo yao, mara zote naamini neno sahihi kwao ni hili YALOPITA YAMEPITA hivi sasa ni maisha baada ya makosa yale.

Kitu kimoja rafiki ambacho kinapaswa kijirudie kichwani mwako ni unaishi leo hauishi jana, ya jana yamepita yamebaki simulizi, unapaswa kusahau huzuni za uliyowahi kupitia, makosa uliyowahi kuyafanya na kumbukumbu za aina yoyote ile zilizopita usiruhusu zikutawale leo, acha kabisa!.

Unaweza kukumbuka tu kama uliwahi kupitia kitu fulani lakini kamwe usiishi katika kumbukumbu hizo, zitaathiri ufanisi na utendaji wako mzuri. The past is GONE!, Close the door.! hakikisha unaufunga vema mlango wa uliyoyapitia na kuufungua mlango ulio mbele yako unaowakilisha wakati huu uliopo.

Pambana sasa acha kukumbuka ya nyuma.

2: UNAPASWA KUSEMA HAPANA.

Ndio sometimes you should say No

Wengi hudhani kukataa ni vibaya na kujikuta wanakubali tu kila kitu mradi aliyemtaka kufanya anamuheshimu au ni mtu anayemuonea aibu, acha sasa niondoe dhana hii kichwani mwako, naomba uamini sasa kuna baadhi ya vitu yakupasa kusema hapana.

-Sema hapana kwa ujumla,
-Sema ndiyo kwa kinachostahili,

Kataa kwa ujumla, sababu yakupasa kuwa na uhakika na nini unahitaji maishani kwani wengi wanaishi kwa bahati mbaya hawajui nini wanapenda kukifanya ambacho kitawaletea mafanikio.

Amua sasa kuchagua kimoja ulicho nacho nakukiwekea mkazo kwa juhudi na maarifa, kamwe usiyumbishwe na mtu akikwambia uache hicho ufuate kile kwa ujumla sema NO itakusaidia kuokoa muda na pia kuwa mfanisi katika kile ulichokiamua.

Hauwezi kutumikia mabwana wawili! hata kazini kwako hakikisha unazingatia kazi yako na sio kumshikia rafiki yako eti kisa amekuomba mwambie NO sababu utapoteza umakini na kazi yako.

Ni njia hii ndio ambayo inafanya waafrika waonekane wababaishaji, unakuta mtu amepeleka maombi ya kazi sehemu amefanyiwa usaili amekubaliwa ghafla bosi anamwambia aanze kazi muda ule na ni muda huo ofisi yake ya zamani ndio anatakiwa aingie, kusema hapana kwa bosi wake mpya anashindwa anajikuta yupo njia panda, au kijana anapenda kuwa mwanahabari lakini baba yake anamtaka asomee uhasibu. kijana anashindwa kusema NO sababu baba amesema.

Acha sasa kama una tabia hii, kuwa na msimamo chagua kitu sahihi chakufanya maishani ili ukiwekee juhudi vyengine sema HAPANA.

Sema ukiwa na uhakika kwamba hutajutia
say "No" Generally
say "yes" very very selectively

Hakikisha unachokikubali ni kweli unaamini ni sahihi katika maisha yako.

"niliwahi kataa kazi ya mshahara mnono sababu ya kujitolea bure kwenye kazi niipendayo" aliwahi sema hivi rafiki yangu fulani ambaye sasa ni mtangazaji mkubwa tu....anasema aliona namna ambavyo kazi ile inamuondoa kwenye ndoto zake zakuja kuwa mtangazaji ndio mana akaamua kuachana nayo.

Je wewe unafanya ukipendacho au kwa sababu ya pesa ndio maana unafanya!? sema hapana ukiwa na mashaka na baadae sema ndio utakapopata uhakika wa nafsi yako na kile unachokikubali.

Mwanasaikolojia maarufu Wilium James kutoka chuo kikuu cha Harvad aliwahi sema "bilief creates the actual fact..

Niliwahi kusoma andiko moja la jamaa mmoja ni msimulizi mahiri wa riwaya, tamthilia na mashairi kutoka Tanzania anaitwa Omar Zongo aliwahi kusema "Mafanikio yapo mbele yako ukipiga hatua za juhudi utakutana nayo"

Ni sahihi kabisa mtazamo huo,kamwe usikate tamaa, maana imeandikwa kukata tamaa ni dhambi.

Kwa vile hatuna muda mrefu hapa acha nikamilishe na kipengele kinachoelezea nguvu ya kutoa.

3: NGUVU YA KUTOA.

Ukweli ni kwamba kutoa ni mada pana na inahitaji kuelezewa kwa kina hasa katika karne hii ya vizazi vilivyo na uhaba wa imani ya kutoa nakujikuta kidogo alicho nacho kumpa mwengine anahisi ni kupoteza, anakumbatia ubahili.

Jambo hili limekaa zaidi kiimani lakini amini lina matokeo chanya kabisa kama ukiliishi.

Vya bure vina gharama sana ndugu yangu, hakikisha unajifunza leo kuhakikisha unatoa kitu chako kulipia huduma yoyote ile.

Unaweza ukawa huna imani na kutoa pesa kumsaidia mtu bila sababu ya msingi basi angalau weka utaratibu wa kumpa mtu kazi japo ndogo tu ili umlipe.

Usilazimishe kila kitu ufanye wewe mwenyewe, hii ni aina ya uchoyo ambayo inawanyima watu wengi baraka. Tengeneza mazingira ya pesa yako ndogo unayoipata kutenga fungu ambalo utahakikisha linawafikia wengine, hii itafanya iwe rahisi Mungu kupitisha pesa kwako na utayaona mafanikio.

Kuanzia leo kama ukikutana na njia inayokuelekeza kutoa basi ifuate maana hiyo ndio njia ya kweli itakayokukutanisha na mafanikio yako ya kweli.

Wenye kuamini maneno ya Mungu watasadiki nikisema kuwa Sadaka yako unayoitoa ndio huenda kuwa ukumbusho kwa Mungu juu ya yale mahitahi yako unayomuomba kila siku.

Katika utoaji wako iwe ni fungu la kumi, Limbuko, Sadaka ya Nadhiri au mchango wowote ule hakikisha unatanguliza imani mbele. Weka matarajio yako kwa Mungu ya kwamba atakulipa maana kwa hakika iliyo kweli imani si kitu endapo mtu hatakuwa na uhakika wa matarajio yake.

Tazama kitabu cha Mwanzo Biblia agano la kale inatuonesha namna ambavyo Habili akiwa na imani thabiti alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini na ikawa chanzo cha yeye kushuhudiwa kuwa ana haki.

Toa ndugu, ipo siri kubwa sana ya mafanikio ambayo imejificha katika ulimwengu huo wa Kutoa.

Na Mungu akubariki sana, ukawe na fikra chanya katika utafutaji wako.

Amiin.
 
Upvote 28
Umepata kula yangu Mlekwa tembelea hii pia
Tayari Mkuu.. shukrani sana
 
Nadhani makala hii haitawahusu vijana wavivu ambao wao wanawaza kuamka nakukaa vijiweni wakipeana mbinu za kupora nakuiba mali za watu.

Hii itawahusu vijana na watu wazima ambao bado wangali kwenye mapambano yakujikwamua nakufikia bango lenye nembo ya mafanikio.

View attachment 1863125

Zipo siri nyingi sana zenye uwezo wakukuvusha daraja kutoka mahali ulipo nakuyafikia mafanikio unayoyaota, nakuyatamani,kila siku watu wanazungumzia kufanya kazi kwa bidii, juhudi na kijituma kuwa ndio nyenzo zakumfanya mtu afanikiwe.

Nakubaliana nazo nyenzo hizo na nyengine nyingi zinazozungumzwa na watu wengi lakini mimi leo nitaongelea tatu tu...

Ya kwanza ni njia ambayo kitaalamu utaitamka kama The Past Is Gone ila mimi nitaiandika kwa kiswahili fasaha kabisa nikiitaja kama YALOPITA SI NDWELE, nyingine ni umuhimu wakusema neno HAPANA na njia ya tatu tutaitazama NGUVU YAKUTOA

1: YALIYOPITA SI NDWELE.

Ni wengi niliozungumza nao kuwapima misimamo yao ya kimaisha walitamka kuhusu makosa ya wazazi wao kuwagharimu katika kutimiza malengo yao...

"baba angenisomesha ningekuwa nimefika mahali fulani"

Wengi husema hivi au wengine hulaumu uzembe wa makosa yao waliyoyafanya shuleni wakiamini kuwa ndio chanzo cha wao kushindwa kutimiza malengo yao, mara zote naamini neno sahihi kwao ni hili YALOPITA YAMEPITA hivi sasa ni maisha baada ya makosa yale.

Kitu kimoja rafiki ambacho kinapaswa kijirudie kichwani mwako ni unaishi leo hauishi jana, ya jana yamepita yamebaki simulizi, unapaswa kusahau huzuni za uliyowahi kupitia, makosa uliyowahi kuyafanya na kumbukumbu za aina yoyote ile zilizopita usiruhusu zikutawale leo, acha kabisa!.

Unaweza kukumbuka tu kama uliwahi kupitia kitu fulani lakini kamwe usiishi katika kumbukumbu hizo, zitaathiri ufanisi na utendaji wako mzuri. The past is GONE!, Close the door.! hakikisha unaufunga vema mlango wa uliyoyapitia na kuufungua mlango ulio mbele yako unaowakilisha wakati huu uliopo.

Pambana sasa acha kukumbuka ya nyuma.

2: UNAPASWA KUSEMA HAPANA.

Ndio sometimes you should say No

Wengi hudhani kukataa ni vibaya na kujikuta wanakubali tu kila kitu mradi aliyemtaka kufanya anamuheshimu au ni mtu anayemuonea aibu, acha sasa niondoe dhana hii kichwani mwako, naomba uamini sasa kuna baadhi ya vitu yakupasa kusema hapana.

-Sema hapana kwa ujumla,
-Sema ndiyo kwa kinachostahili,

Kataa kwa ujumla, sababu yakupasa kuwa na uhakika na nini unahitaji maishani kwani wengi wanaishi kwa bahati mbaya hawajui nini wanapenda kukifanya ambacho kitawaletea mafanikio.

Amua sasa kuchagua kimoja ulicho nacho nakukiwekea mkazo kwa juhudi na maarifa, kamwe usiyumbishwe na mtu akikwambia uache hicho ufuate kile kwa ujumla sema NO itakusaidia kuokoa muda na pia kuwa mfanisi katika kile ulichokiamua.

Hauwezi kutumikia mabwana wawili! hata kazini kwako hakikisha unazingatia kazi yako na sio kumshikia rafiki yako eti kisa amekuomba mwambie NO sababu utapoteza umakini na kazi yako.

Ni njia hii ndio ambayo inafanya waafrika waonekane wababaishaji, unakuta mtu amepeleka maombi ya kazi sehemu amefanyiwa usaili amekubaliwa ghafla bosi anamwambia aanze kazi muda ule na ni muda huo ofisi yake ya zamani ndio anatakiwa aingie, kusema hapana kwa bosi wake mpya anashindwa anajikuta yupo njia panda, au kijana anapenda kuwa mwanahabari lakini baba yake anamtaka asomee uhasibu. kijana anashindwa kusema NO sababu baba amesema.

Acha sasa kama una tabia hii, kuwa na msimamo chagua kitu sahihi chakufanya maishani ili ukiwekee juhudi vyengine sema HAPANA.

Sema ukiwa na uhakika kwamba hutajutia
say "No" Generally
say "yes" very very selectively

Hakikisha unachokikubali ni kweli unaamini ni sahihi katika maisha yako.

"niliwahi kataa kazi ya mshahara mnono sababu ya kujitolea bure kwenye kazi niipendayo" aliwahi sema hivi rafiki yangu fulani ambaye sasa ni mtangazaji mkubwa tu....anasema aliona namna ambavyo kazi ile inamuondoa kwenye ndoto zake zakuja kuwa mtangazaji ndio mana akaamua kuachana nayo.

Je wewe unafanya ukipendacho au kwa sababu ya pesa ndio maana unafanya!? sema hapana ukiwa na mashaka na baadae sema ndio utakapopata uhakika wa nafsi yako na kile unachokikubali.

Mwanasaikolojia maarufu Wilium James kutoka chuo kikuu cha Harvad aliwahi sema "bilief creates the actual fact..

Niliwahi kusoma andiko moja la jamaa mmoja ni msimulizi mahiri wa riwaya, tamthilia na mashairi kutoka Tanzania anaitwa Omar Zongo aliwahi kusema "Mafanikio yapo mbele yako ukipiga hatua za juhudi utakutana nayo"

Ni sahihi kabisa mtazamo huo,kamwe usikate tamaa, maana imeandikwa kukata tamaa ni dhambi.

Kwa vile hatuna muda mrefu hapa acha nikamilishe na kipengele kinachoelezea nguvu ya kutoa.

3: NGUVU YA KUTOA.

Ukweli ni kwamba kutoa ni mada pana na inahitaji kuelezewa kwa kina hasa katika karne hii ya vizazi vilivyo na uhaba wa imani ya kutoa nakujikuta kidogo alicho nacho kumpa mwengine anahisi ni kupoteza, anakumbatia ubahili.

Jambo hili limekaa zaidi kiimani lakini amini lina matokeo chanya kabisa kama ukiliishi.

Vya bure vina gharama sana ndugu yangu, hakikisha unajifunza leo kuhakikisha unatoa kitu chako kulipia huduma yoyote ile.

Unaweza ukawa huna imani na kutoa pesa kumsaidia mtu bila sababu ya msingi basi angalau weka utaratibu wa kumpa mtu kazi japo ndogo tu ili umlipe.

Usilazimishe kila kitu ufanye wewe mwenyewe, hii ni aina ya uchoyo ambayo inawanyima watu wengi baraka. Tengeneza mazingira ya pesa yako ndogo unayoipata kutenga fungu ambalo utahakikisha linawafikia wengine, hii itafanya iwe rahisi Mungu kupitisha pesa kwako na utayaona mafanikio.

Kuanzia leo kama ukikutana na njia inayokuelekeza kutoa basi ifuate maana hiyo ndio njia ya kweli itakayokukutanisha na mafanikio yako ya kweli.

Wenye kuamini maneno ya Mungu watasadiki nikisema kuwa Sadaka yako unayoitoa ndio huenda kuwa ukumbusho kwa Mungu juu ya yale mahitahi yako unayomuomba kila siku.

Katika utoaji wako iwe ni fungu la kumi, Limbuko, Sadaka ya Nadhiri au mchango wowote ule hakikisha unatanguliza imani mbele. Weka matarajio yako kwa Mungu ya kwamba atakulipa maana kwa hakika iliyo kweli imani si kitu endapo mtu hatakuwa na uhakika wa matarajio yake.

Tazama kitabu cha Mwanzo Biblia agano la kale inatuonesha namna ambavyo Habili akiwa na imani thabiti alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini na ikawa chanzo cha yeye kushuhudiwa kuwa ana haki.

Toa ndugu, ipo siri kubwa sana ya mafanikio ambayo imejificha katika ulimwengu huo wa Kutoa.

Na Mungu akubariki sana, ukawe na fikra chanya katika utafutaji wako.

Amiin.
Vote no 8 Environmental Security
Pamoja sana
 
Hii hata kwente vitabu vya dini imesemwa, the more you give, the more you receive
Yes.. ni njia nzuri sana ya kufikia Mafanikio.. na wengi wanafahamu hilo sema ni ngumu sana kuifanyia kazi.. na hapo ndipo tunapofeli wengi..
 
Kutoa ni imani, kama hana imani ya utoaji basi hata kanisani sadaka ataona ubahili kutoa, nadhani umaskini wetu pia unachangia watu kufeli kwenye kutoa
 
Hapo Kwenye nguvu ya kutoa ni mada pana kidogo kama nilivyosema hapo juu, but tunachopaswa kujua ni kwamba kutoa si lazima uwe na kingi hata unapotoa Kweny kile kidogo ulichonacho kwa moyo wa kupenda na kwa imani ndipo unapobarikiwa na kufanikiwa zaidi, lakini pia kutoa si lazima iwe pesa, kama nilivyoeleza Kwenye andiko kama unaona ni shida kutoa pesa basi ajiri wenzio na uwalipe kutokana na kazi watakayoifanya, Lakini pia unaweza ukatoa hata SADAKA YA MUDA WAKO katika kuwaelekeza watu, kuwashauri na kuwafundisha cha kufanya ili waweze kufanikiwa mbona pia utakua umesaidia wengi, Mimi nashangaa sana watu wanavyokua na choyo hata kwa habari ya kutoa maarifa kwa wenzao Kueleza njia walizopita mpaka kufanikiwa mara nyingi sana ushuhuda ndio huwa unamtoa mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine wala si pesa.. Kuna mengi sana ya kuyafahamu katika utoaji ila ngoja niishie hapa... Wangapi wanakubaliana na mimi katika hili!? Drop comments yako hapa na me nitapita nayo..
 
Karibu kwa maoni rafiki.. zaidi NAOMBA sana kura yako.. sehemu ya kupiga kura iko chini ya andiko langu utoana neno Vote na alama ^ wewe utabofya tu hiyo alama na uhakikishe namba ya kura imeongezeka... Asante sana
 
Back
Top Bottom