Ushauri

Joined
Apr 29, 2018
Posts
30
Reaction score
17
Habari za Jioni Wakuu...! Poleni na Harakati za kutafuta ridhiki niende moja kwa moja kwenye mada husika

Mimi nilikuwa na shemeji yanu tulikuwa tumezoeana ile mbaya Yani ikafikia wakati Mpaka Ndugu yangu akagombana na Mimi baada ya hali hiyo kutokea Mie sikutaka yajirudie tena nikaamua kuacha mazoea na shemeji Niliyakata ghafla na Mimi nilimwambia baada ya kufanya ivyo alianza kunichukia na kuniona mnafiki Kwakua nilijenga mazoea na mshikaji aliyekuwa rafiki yake, Alikuwa akipita dirishani anaongea maneno ambayo hayana staha kama hauna uvumilivu unaweza ukampiga lakini nilipiga moyo konde na kusema yatakwisha

Leo nimerudi zangu nyumbani Nimefika najiandaa kwenda kuoga Mara nasikia yule Mwanamke amepigwa nikasema Kwakua amepata tatizo ngoja nikamjulie hali ile nafika Tu Anaanza kwanza kunicheka sikujali nikauliza imekuaje akaniambia hamna kitu ,Nikauliza tena umeumia akaniambia hajaumia ,Nikasema aliyekupiga ni mwanamke au Mwanaume? akaniambia Mwanaume Hatujapigana Bali Tumegombana Mi nikaona haina shida majibu yake nikaona haitaji Msaada wangu hata kidogo Mi nikaondoka ile nafika Ndani Tu nikamsikia anapita anasema " Mi sijapigana Wambea wa mtaa mnataka Muende mkanitangaze" Aise roho iliniuma ila nikaona sasa imetosha

Nilikuwa Naomba mawazo yenu Je, Mtu kama huyu akipata shida unamsaidia au unamuacha Apambane na Hali yake KWA sababu Mi siwezi kumfuata Mimi ni Mwanaume Nina kifua na koromeo sitaki kugombana na mwanamke...!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…