Ushauri

Ushauri

MTIRO

Senior Member
Joined
May 5, 2012
Posts
120
Reaction score
16
Wana jukwaa kwanza nianze kwa kuwasalimu, naimani wikiend ilikuwa nzuri na mmejiandaa vema kuianza wiki. Binafsi namshukuru mwenyezi mungu mwingi wa rehema kwani kiafya nipo vizuri.
Lengo kuu la makala hii ni kuomba ushauri. Niaze kwa kujieleza mimi binafsi, mi ni miongoni mwa wahanga waliokosa ajira toka nilipohitimu masomo yangu mwaka 2011. Sasa nimejitahidi sana kupata mtaji wa kufanya biashara ila nadhani kama mnavyofahamu mazingira ya mikopo Tanzania yalivyo. Hivyo basi nimejitahidi kupata sh million moja. Sasa ushauri ninao uomba ni niifanyie nini hii pesa ili isipotee??
 
  • Thanks
Reactions: BIR
Kwanza inabidi kuangalia eneo ulipo na fursa zilizopo pia,
 
Tuwasiliane 0759601820 au 0714306015 mimi pia ni tuone tutasaidianaje!! nipo Dar
 
Back
Top Bottom