Ushawahi jiuliza kwanini una nywele fupi na mwenzio ana ndefu

Ushawahi jiuliza kwanini una nywele fupi na mwenzio ana ndefu

Joined
Jul 9, 2015
Posts
23
Reaction score
2
Umewahi kujiuliza kwanini kuna watu nywele zao huota na kua ndefu lakini wengine nywele zao zinaonekana kama hazioti?
>Kila Nywele hupitia hatua tatu muhimu katika mzunguko wa uhai wake.

1) Anagen- Nywele huota na kuongezeka urefu na kipindi hiki kinadumu kati ya miaka 2 hadi 8. Kipindi kikiwa kirefu nywele nazo hua ndefu. √Asilimia 80 ya nywele kichwani ziko katika hatua hii na nywele hizo huongezeka urefu wa wastani sentimeta 1 ndani ya mwezi mmoja.

2) Catagen -Ni hatua ya nywele kupoteza uhai na hatimaye kudondoka na inadumu kwa wiki 2. Wastani wa asilimia 1 ya nywele kichwani ziko catagen.

3) Telogen- Mwishoni nywele mpya chini ya ngozi huandaliwa na hatimae huchomoza ambayo inadumu miezi 2-3. Asilimia 20 ya nywele ziko hatua hii.

Binadamu ana wastani wa nywele laki moja kichwani. Nywele kuwa ndefu au fupi hutegemea na wewe ulivyorithi na urefu wa kipindi cha Anagen. Hamna kitu chochote utakacho eka kwenye nywele zako kwa nje ambacho kitasaidia ziote haraka...cha muhimu ni kua na afya na lishe nzuri na kuzitunza nywele vizuri ili zisikatike.

Naomba unifollow kwenye account yangu ya Instagram...@ daktari_sundae
 

Attachments

  • IMG_20150709_101227.jpg
    IMG_20150709_101227.jpg
    21 KB · Views: 186
kumbee ngoja nipunguze bajeti ya kupaka madude kwenye nywele zangu
 
Miss Chaga...ongeza bajeti upande wa chakula, na kucheki afya. Stress ya aina yeyote pia hufanya nywele kuingia kwenye catagen stage.
 
Back
Top Bottom