Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Nitag basi meneja.
Unakumbuka nilionana na wewe Nyamagana stand ukanumwagia maji,ukaja ofisini Pale Bank,na bulk money zako za mauzo ukakutana na mimi Meneja!

Mayan nilishushuka mwee
 
Angalau tupate kastori kwa ukweli kidogo tupumue[emoji39]
 
Kuna watu wanafanya kufuru kwenye matatizo ya wenzao mpaka unajiuliza hivi hawa kesho yao wanaijua vizuri eeh!!! Pole sana maana nahisi maumivu uliyopata
Dah! Nilikuwa nawachukia sana. Uzuri ndugu tulipeana zamu yakukaa na mgonjwa ila ilikuwa ukifika zamu yangu nahisi naenda jela. Washukuru Mungu mzee ni mkali sana ko japo alikuwa mgonjwa ila nilikuwa namuogopa laa sivyo ningekuwa nishawazaba vibao siku nyingi
 
waazimaji ndivyo walivyo fix nyiiingiiii 😂 😂 😂
 
Kuna parking fulani pale Msewe siku hiyo naenda kupark kigari changu Corona saloon kimechoka choka kidogo tupo na rafiki yangu. Pale karibia na geti kukawa na dada mmoja anaelekea tunako elekea lakini kama yupo barabarani zaidi. Mimi nikaona kama anaringa nikamsogezea bodi kimtindo. Akasogea pembeni kwa utulivu. Wakati nataka kushuka kufungua geti akatufungulia na hakutusemesha kitu pamoja na kafujo niliyo mfanyia kwani alikuwa amevaa kikawaida kama msichana wa mtaani. Nimeingia ndani kupark kumbe yeye alikuwa anakuja kuchukua gari lake. Ile kushuka namuona anatoka na V8 zito. Nilisikia aibu sana tuka tazamana na rafiki yangu tukashangaa kwani yule dada hakuonesha mbwe mbwe zozote. Nilisikia vibaya sana kumdharau yule dada.
 
[emoji16][emoji16][emoji16] umeamua kutetea akina dada, hakika umekuja kitofauti
 
Akina dada ndiyo walio shambuliwa sana ktka huu uzi kila mtu anamtupia lawama mwanamke, ndiyo maana nikasema amewatetea akina dada.
Ukisema wameshambuliwa tayari ushaweka walakin kuwa yaliyoandikwa hayana uhalisia..

Pia dhana ya kutetea haipo kama lengo la huu uzi ni kutoa ushuhuda sioni kama hayo maneno "Kushambulwa na Kutetewa yanapaswa kutumika...

Kumbuka huu si mdahalo kati ya wanawake na wanaume hebu jikite kwenye kichwa chako cha uzi...
 
Sawa mkuu kwa kuliona hilo.
 
Uliyajuaje mazungumzo yao au jamaa yako alikusimulia?
 
Kuna watu wanadharau alafu kuna hawa mareceptionist kwenye maofisi, unaweza dhani kuna kacourse maalum ka dharau wamesomea na kukafanyia field.

Niliwai tafutwa na kamicrofinance fulani kwa ajili ya kufanya nao kazi zama zile za mkwere. Sasa siku nmeripot kwa ajili ya kuonana na HR na MD nimejibebea kabahasha kangu ka vyeti na cv nimejivalia casual shirt jeupe na denim jeans ya blue. Nmefika kwa receptionist nmemsalimia vizuri kajibu, kumuuliza kuhusu hr ndio balaa lilipoanza. Nakumbuka alijibu hatuna nafasi za kaz sasa hv subiri tukitangaza, nikamwambia sijaja kuomba kazi, akaniuliza bahasha ya nini? Nikajibu ukweli ina vyeti, nikapewa bonge la sonyo. Gafla stuff mwingine akawa anapita akamwita kishambenga ili waje wanizodoe vizuri. But yule mwenzie alkua mstaarabu aliniuliza kama nna appointment na HR nikajibu MD ndio kanielekeza nionane na HR. Basi akaenda kuniitia, nikaitwa kwa HR nikasign contract nikapewa na mtu wa kunionyesha mazingira .

Orientation nilianzia floor ileile nimefika kwa yule dada, jamaa akamuuliza J.... Umemuona Head of internal audit mpya. Dah niljikuta namuonea huruma gafla maana alijitafuta pale kwenye meza yake hadi sio poa. Basi akaanza kujilegeza kila akiniona hadi nikaanza kuhisiwa vibaya. Nashukuru Mungu nilifanikiwa kumkwepa had contract ilipoisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…