Ushawahi kufeli katika biashara?

Ushawahi kufeli katika biashara?

Ibrahimeliza

Member
Joined
Nov 25, 2020
Posts
37
Reaction score
26
Watu wengi wanaanzisha biashara lakini wengi pia wanafunga biashara, sababu na shauku ya kuanzisha biashara mara nyingi ndio hiyohiyo ya kufunga biashara ila nina wazo au kanjia kadogo ambacho labda kanaweza kukusaidia.

Kama umefeli katika biashara yako, swali la msingi kujiuliza nimefeli mara ngapi katika biashara hii...?? Nafanya mimi tu hii biashara...?? Wenzangu wanawezaje kufanikiwa katika biashara hii...??

Wazo langu ni hili, ukiona unafeli katika biashara au biashara yako inakuwa ngumu au unahisi inaenda kuanguka basi kabla ya kubadilisha biashara, jaribu kubadilisha mfumo au namna ya ufanyaji wako wa biashara wazungu wanaita (approach) kila biashara inachangamoto zake kwahiyo kama hautaweza kuisimamisha biashara hata moja mpaka ikakua basi utakuwa unaishia kuanzisha na kufunga kama wengi wanavyofanya.
 
Niliwahi fanya biashara ya play station, nilikuwa nalaza 30,000 per day normal week day na hadi 70,000 per day week end.

Akaibuka mzee fulani kastaafu kapata hela zake za redandasi akafungua PS kubwa hiloo akaweka matv kibaao mbaya zaidi ni kwenye fremu ya nyumba zake, madogo wakaambizana wakaniacha na mativii yangu.
Nikaishia kufunga.
 
Nishafail mara mbili, biashara ya mitumba na biashara ya Nazi toka Mafia
 
Niliwahi fanya biashara ya play station, nilikua nalaza 30,000 per day normal week day na hadi 70,000 per day week end,
Akaibuka mzee fulani kastaafu kapata hela zake za redandasi akafungua ps kubwa hiloo akaweka matv kibaao mbaya zaidi ni kwenye fremu ya nyumba zake, madogo wakaambizana wakaniacha na mativii yangu.
nikaishia kufunga.

Haha pole sana mzee.
 
Hahahahahaaa pole sanaaaa, ila uzuri wake unaweza ukaanzisha sehemu nyingine na kufanya vizuri zaidi,
 
Kuanza biashara Ni rahisi, kuiendeleza na kuikuza Ni ngumu, ila kuikuza na kuendelea kukua Ni swala lingine ilo
Kweli kuna biashara nyingi zinafeli kwakushindwa kuikuza hiyo biashara, kuikuza hiyo biashara inahitaji ujuzi mwingine sio ule ambao umeutumia kuanzisha biashara, hapo ndio tunaposhindwa.
 
Nishafail mara mbili, biashara ya mitumba na biashara ya Nazi toka Mafia
Kitu kizuri katika biashara unajifunza kwa vitendo kwhy ili ujue kosa lako lazima ukosee, cha msingi sio kufeli tu katika biashara cha msingi kujua kilichosababisha kufeli husipo jua kilichokufanya uanguke kila ukipita njia hiyo basi kitakuangusha kila ukipita,
 
Nimefanya uchunguzi mdogo biashara nyingi zinakufa kwa sababu ya ;
Usimamizi mbovu,
Mtaji mdogo ususani pale unapotokea ushindani,
Serikali kupitia sheria zake,
Mambo ya asili kama mvua,
Kukosekana kwa elimu ya kutosha katika biashara ususani kwenye kupanga gharama , namna ya kununua bidhaa kwa bei nzuri,
Na
Kuwapo kwa vishoka au madalali katika manunuzi na uuzaji wa bidhaa husika.

Sent from my Nokia G10 using JamiiForums mobile app
 
Kitu kizuri katika biashara unajifunza kwa vitendo kwhy ili ujue kosa lako lazima ukosee, cha msingi sio kufeli tu katika biashara cha msingi kujua kilichosababisha kufeli husipo jua kilichokufanya uanguke kila ukipita njia hiyo basi kitakuangusha kila ukipita,
Ni kweli mkuu, kila aliefanikiwa bas jua huko nyuma alianguka mahala ila alihazama wapi alijikwaa then akarekebisha akasonga mbele
 
Kufeli kwenye biashara ndio njia ya kujifunza na kujua vitu gani vinafanya kazi na vitu gani havifanyj kazi
 
Back
Top Bottom