Kuna mambo matatu
1. Kuna namba unasave kwa muda kwa matumizi maalumu kisha unasahau kuifuta ukimaliza jambo lako. Nyingine unasave lakini mtu huyo hamuwasiliani kitambo mpaka unasahau hata hilo jina wakati ulisave mwenyewe
2. Majina mengine yanakuwa kwenye simu uliyoweka laini yako mfano simu za kununua bila kurestore (japo hii ni kwa wachache sana wasio na uelewa mpana wa simu). Mara nyingine simu za kutumia pamoja na wengine, unakuta umempa mtu akatumie kwa muda anaenda kusave baadhi ya contacts zake humohumo
3. Kulog in kwenye email tofauti na inayotumika ndani ya simu yako kunasababisha majina ya kwenye email hiyo kuingia kwenye simu yako. Tena hili jambo huwa linabadili hata baadhi ya majina uliyosave sijajua ni kwamba hiyo namba ipo kwenye emails zote mbili ndiyo maana inajikoroga au vipi, unakuta namba ulisave mfano NICE imebadilika na kuwa NICE De NICE au ulisave herufi ndogo lakini Unakuta ipo kwa herufi kubwa
Yote kwa yote kama jina hukusave wewe kwenye simu yako utaligundua tu lazima. Binafsi huwa nagundua kwa namna nyingi na sipuuzi mpaka nipate kujiridhisha limeingiaje ndipo nitulie. Kwa mfano contacts zangu huwa herufi za kwanza tu ndio kubwa, sina vifupisho zaidi ya vile ambavyo ni rasmi katika lugha mfano Dr. Mh. Eng. Prof. Mwl. Shk. nk, namba za matukio naweka jina kwa kuzingatia tukio mfano nimenunua kitu kariakoo nitaweka "Juma Friji-Kariakoo", nazingatia sana ufasaha wa lugha mfano huwezi kuta nimeweka "polis/polic" kumaanisha "polisi/police".
Kwa staili hiyo nikikuta namba siielewi inakuwa ni rahisi kugundua kama ni yangu au siyo yangu japo kuna zile za kusave kajina kamoja tu huwa zinanitesa. Unakuta umeandika jina moja tu Shabani kwa kujiamini kwamba Shabani ni mmoja tu kwa simu sasa ngoma inakuja umemsahau huyo Shabani ni nani na ilikuwaje ukawa na namba yake