ushawahi kumbwa na dhoruba ukiwa peke yako

ushawahi kumbwa na dhoruba ukiwa peke yako

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
nakumbuka siku moja nimetoka singida naenda manyara kwa baiskel ilikuwa ni masika,

nikiwa katikati ya mbuga ilikuja mvua ya ghafla ambayo sikuitarajia kurudi nyuma ni mbali na ninapokwenda ni mbali ikabidi nikomae tu hivo hivo basi bhana,

baiskel ikabana matope kwenye madgad ikawa haitembei nikatafuta hata jiwe ili niivunje ile madgad maana hata kijiti kutolea matope nilikosa kila hatua nikinyanya viatu vinabakia chini ikabidi viatu nikatemana navyo nikapiga pekupeku,

ile mvua ilinyesha zaidi ya lisaa limoja lakini huo msoto wake mungu tu alisaidie mvua isikie tu ukiwa ndani lakini siku ikikukuta maeneo mbaya, sio mchezo,

japo nilitoboa safari yangu ila niliugua siku tatu,
 
Mvua ya mawe unaijua mkuu ilinikuta natoka Bariadi kwenda Mallya ngoma ikaanza niko kwenye kisehem hakina watu ilinipiga nikajaribu kujificha kwenye mti lakini mado mawe yanagonga Mungu mkubwa ilikata ila nilikua natetemeka hata basiekeli kuikokota nashindwa kuna mzee nae alikua nyuma akaniona navo oata shida akanisaidia mpaka kwenye mji wa mtu wakanipeleka jikoni na mama mwenye mji akapika uji maana hadi meno yalikua yanagongana mvua ili ilijua gahafla ina upepo na mawe hapana sijawahi ona.
 
Back
Top Bottom