Ushawahi Kutana na tangazo gani la biashara likakuacha na mshangao

maccavel

Member
Joined
Jan 17, 2025
Posts
40
Reaction score
76
Wakuu, katika harakati zetu sisi vijana, hasa upande wa kibiashara, je, ubunifu wa kutengeneza matangazo una athari zozote katika maendeleo ya biashara zetu?

Kwa mfano, unakuta baadhi ya watu huweka matangazo yenye vichekesho, na baadhi yao huweza kuvutia wateja na kuwafanya wapendezwe na kujiunga na biashara yako.

Aidha, baadhi ya vijana hubuni matangazo yanayoendana na kizazi chetu (Gen Z). Mathalani, matangazo mengi ya Gen Z huwa na lugha ya mzaha au wakati mwingine maneno yasiyo rasmi; ingawa mara nyingi huvutia hadhira ya vijana pekee, huacha hadhira ya watu wazima na wazee kuipita biashara husika.

Kwa mfano, leo katika pita pita zangu ndani ya Jiji la Dar es Salaam, nilikutana na mwanadada mlimbwende kweli akiwa ameshika kontena lake lenye korosho, na mkono mwingine akiwa amebeba kipaza sauti kinachosema:
“Hello, nauza korosho mia tano, mia tano, lakini namba za simu sitoi!”

Kwa hakika, tangazo hili si mimi tu bali liliwaacha watu wengi katika hali ya mshangao na pia kucheka, jambo lililonipelekea mimi na wenzangu kununua korosho zile.

Ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu kwamba tunapobuni matangazo, tuhakikishe hatubagui hadhira — vijana, watu wazima na wazee — ili biashara zetu ziweze kukua zaidi.

Mwisho kabisa, vipi wewe mdau? Umewahi kukutana na tangazo gani la biashara lililokuacha katika hali ya mshangao? Na una ushauri gani kwa vijana wenzako kuhusu ubunifu wa matangazo?
 
Attachments

Kuna mshangazi Buguruni hapa unauza mahindi ya kuchemsha na Karanga, ana tako mpaka anatembea huku analikokota.
Sasa anapita anaita "mahindi ya kuchemsha na karanga, sehemu ya kumwaga ipo"

Kidogo nitupie swaga, ila ana madeni taasisi zote za mikopo, uswahilini mpaka ushuani,
Nikaona hapa nitapoteza malengo acha Nile Kwa macho
 
Hahahaha kwahy mkuu,huyo mshangazi ana sehemu ya kumwaga, hahahaha
 
Wakuu, katika harakati zetu sisi vijana, hasa upande wa kibiashara, je, ubunifu wa kutengeneza matangazo una athari zozote katika maendeleo ya biashara zetu?

Kwa mfano, unakuta baadhi ya watu huweka matangazo yenye vichekesho, na baadhi yao huweza kuvutia wateja na kuwafanya wapendezwe na kujiunga na biashara yako.

Aidha, baadhi ya vijana hubuni matangazo yanayoendana na kizazi chetu (Gen Z). Mathalani, matangazo mengi ya Gen Z huwa na lugha ya mzaha au wakati mwingine maneno yasiyo rasmi; ingawa mara nyingi huvutia hadhira ya vijana pekee, huacha hadhira ya watu wazima na wazee kuipita biashara husika.

Kwa mfano, leo katika pita pita zangu ndani ya Jiji la Dar es Salaam, nilikutana na mwanadada mlimbwende kweli akiwa ameshika kontena lake lenye korosho, na mkono mwingine akiwa amebeba kipaza sauti kinachosema:
“Hello, nauza korosho mia tano, mia tano, lakini namba za simu sitoi!”

Kwa hakika, tangazo hili si mimi tu bali liliwaacha watu wengi katika hali ya mshangao na pia kucheka, jambo lililonipelekea mimi na wenzangu kununua korosho zile.

Ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu kwamba tunapobuni matangazo, tuhakikishe hatubagui hadhira — vijana, watu wazima na wazee — ili biashara zetu ziweze kukua zaidi.

Mwisho kabisa, vipi wewe mdau? Umewahi kukutana na tangazo gani la biashara lililokuacha katika hali ya mshangao? Na una ushauri gani kwa vijana wenzako kuhusu ubunifu wa matangazo?
Chai
 
Bango la biashara la ccm"Chagua Samia, kazi iendelee"
 
Back
Top Bottom