Ushawahi Kutapeliwa?

Pole sana mkuu Kumbe hua wanatumia na dawa kufanya mazingira.
Mimi nikajua hua ni ujanja tu wakati wa kubadili ili kumukabidhi muhusika.
 
[emoji1787][emoji23] Daah

yani pamoja na ukaguzi na upembuzi yakinifu lkn wahuni wakakufanya vibaya.
 
Pole sana mkuu Kumbe hua wanatumia na dawa kufanya mazingira.
Mimi nikajua hua ni ujanja tu wakati wa kubadili ili kumukabidhi muhusika.
kabisa, mimi mwenyewe nilifikiri hivyo ( yaani wanatumia janja janja tu)
 
Nilipanda basi stand mpya bana
Nikaona ili nisiwe bored kwenye basi ngoja ninunue magazeti ntasoma njiani

Ilikua Ijumaa Nikanunua magazeti kama 6 hivi nilipo taka kuja kuyasoma sasa nakuta magazeti matatu ni ya mwaka majuzi sijui ila ya Ijumaa [emoji23][emoji23]
 
Kwanini usingeenda kwenye ofisi zao hao wenye basi??.
 
Nishawahi tapeliwa Buguruni nikiwa mdogo almost 14 years, niko mishe mishe naenda kumpa hi dada mmoja pale Buguruni Rosana kama sijakosea, akatokea Jamaa mmoja ng'ambo ya barabara akanifata, tukaanza piga story akajitambilisha yeye ni askari na kuna Benki kariakoo imeibiwa, hivyo pesa zilizoibwa znatafutwa.

Jamaa akatoa ID fake akanionesha hata ckuangalia vzuri akairudisha mfukoni, akasema twende Buguruni karibu na darajan pale Mpakani mwa Ilala/Buguruni.

Wakati tunaenda akamuita na kijana mwingine pia akamueleza kama alivonieleza mie tukawa watatu.

Tumefika hayo maeneo tajwa juu, akachukua pesa za jamaa, baada ya dakika chache sana akamrudishia akasema zake hazina shida.

Akachukuaa pesa zangu pamoja na simu tecno lain 2 cjui 3, akasepa navyo ng'ambo ya pili, akinitaka nisubirie akachek kama zile pesa sizo zilizoibiwa bank kariakoo,

Baada ya muda kidogo akili inakuja Kwann nimpe simu, wakati zmeibiwa Hela, nkaanza kucheka nimeibiwa simu pamoja na 20k ya viatu vya shule.
Nikaja gundua yule jamaa mwingine kumbe walikuwa wote na alifanya kuchukua pesa za mwenzangu kwanza Ilikuniaminisha.

Karibu Dar es Salaam
 
Siku nyingine, nimeenda Ubungo kumsalimia jamaa yangu anayeuza mayai stendi ya Ubungo, hii ni 2015 hivi.

Tuko chini pale darajani akaja mzeee wa makamo akawa anapiga story na mwenzangu, jamaa akaniambia ni chill huku akiongea na yule Mzee baada ya muda kidogo akarudi akiwa kachanganyikiwa.

Kumuuliza jamaaa alimuomba simu ye akampa ndo ikawa ntolee, inasemekana jamaa alipiliziwa dawa, sasa dawa zimekuja kuisha anashtuka kaibiwa.

Aliyemuibia alikuwa ni mtu maaarufu pale kijiweni, siku kadhaa akaja akadakwa na polisi
 
Siku naenda Kununua mahitaji ya shule advance, nikawa natembea mitaa ya Ubungi darajani uelekeo wa Tabata, nikakuta vijana wanacheza mchezo wa karata kwenye mezaa, nikasimama kucheki namie nikaona mbona easy na watu wanashinda.

Namie nikashawishiwa na jamaa za pale nicheze, nikaambiwa niweke 10k nikipata nachukua na Hela Yao, kweli nimecheza mara ya kwanza nikapata.

Jamaa akasema umeweza lakin unatakiwa ucheze mara2 nkasema sawa, kucheza mara ya pili, ile nataka kushika karata YENYEWE Kun mjinga alinipiga Kofi kuja kuchagua karata jamaa ashabadirisha, nikawa nimeliwa.

Ikabidi nitoe Hela niwape, ikumbukwe hapo nlikuwa naenda nunua baadhi ya vitu vya shule mfukoni nlikuwa na laki na kidogoo, wakati naingiza mkono Ili nichukue 10k Moja niwape wale jamaa wakaanza nizonga nitoe Hela zote, mmmoja akaingiza mkono akatoa pesa yote wakachukua na kunambia niondoke.

Kama kuna siku nliyopata jaziba na kutaka nipigane na kundi la watu nisio waweza nisiku ile, nkatoka hapo wananitisha kunichukulia simu na viatu vyangu, nikawawakia kinomaa lakin ndohivo pesa imeenda.

Nikasogea pemben jamaa mmoja akasema twende chin ya daraja akanipe dawa ni reverse pesa zirudi nikamuona mshenzi tu nikagoma akaniacha. Ila huyu jamaa alichonishangaza alinitajia mtu mmoja wa nyumbani bush ambae namjuaa kabisa nikahisi ni mchawi labda.

Tokea siku hiyo nikiona magenge ya kucheza karata napitiaa mbali kabisa, wale jamaa ka jinsi nlivyopatwa na jaziba ningekuwa na bastola nlikuwa naua wote pale.

Sikuhizi kijiwe kile hakipo, it is about 6 yrs back since this event occurred.

SIJAWAHI ibiwa Tena wala tapeliwa Tena mji wowotee ule Tz
 
Pole sana mkuu Kumbe hua wanatumia na dawa kufanya mazingira.
Mimi nikajua hua ni ujanja tu wakati wa kubadili ili kumukabidhi muhusika.
hakunaga madawa kwenye utapeli otherwise wangekua mabilionea wakutupwa kama kuna dawa zinafanya hizo kazi.ni mathematics tu
 
Pole mkuu
 
hakunaga madawa kwenye utapeli otherwise wangekua mabilionea wakutupwa kama kuna dawa zinafanya hizo kazi.ni mathematics tu
Madawa yapo mkuu..
Kuna dogo alikuwa anasoma chuo ATC katoka kutembea maeneo ya levolosi primary kakutana na mhuni sielewi ilikuwaje
kitu kama walisalimiana kwa kushikana mikono,
dogo kamuachia begi alilokuwa amebeba na kaijia na simu yake hostel iliyokuwa chaji kampelekea mhuni aliyemuacha
nje ya geti course huwezi ingia bila kitambulisho.
Anarudi hostel ndio anasema ameibiwa na alikuwa out of control alikuwa anafanya chochote anachoambiwa na jamaa.
 
Ngoshaaaa
 
Wapo kibiashara haijalishi yashapitwa na wakati wao wanaweka sokoni tu.
Hizi ndio Biashara za town
 
Kweli huu wizi ulishamili sana na wanatumia wenzao kuwaaminisha.
 
Hii ya kutumia dawa ipo sana yaani unaweza kumpeleka mpaka Nyumbani kwako ili akakuibie vizuri.
 
Kweli maana tunajifunza kutokana na makosa kwa sasa vitu kama hivyo sizani kama vitatikea tena kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…