Ushawahi kwenda kwa mganga?

Ndio nilienda ila gharama niliyotumia ni bora ningenunua kile nilichopoteza kwa kuibiwa.
 
😂😂😂😂😂😂😂
 
[emoji3][emoji3] Kuna dada aliibiwa simu akaenda kwa mganga wa tv akamwona mwizi wake na akarudishiwa simu
Mkuu Waganga wa TV ni wachache sana kwa sasa , % kubwa yao MATAPELI ndio walee kila nguzo za Umeme utakuta tangazo "Mganga kutoka sumbawanga"
 
Huyo dada atakuwa ameingiliwa na pepo aangalie vizuri hizo dawa hufanya kazi na mapepo.
 
Waganga wa kienyeji matapeli sana
 
Pakitokea wizi siwezi kukubali upumbavu wa kuleta mganga eti atumie madawa yake kujua mwizi, hichi kitu hakipo katika imani yangu.

Hayo madawa wanayokupaka saa nyingine yanakuja kukuletea matatizo makubwa zaidi (kukuroga)

Hao watu sio wa kuamini,
Mtu kashaibiwa, halafu anajipeleka kuibiwa tena kwa mganga.
 
Nimewahi kunywa hio dawa,wakati tunarudi home niliona viumbe wengi sana, tunaoonekana viumbe ni vichache kuliko visivooneka
 
Ni kweli waganga wengine ni matapeli, lakini uchawi upo na nguvu za giza zipo!

Nimeona uchawi kwa macho yangu mawili!
Uchawi ni nini na utajuaje huu ni uchawi na si utapeli tu au kitu ambacho si uchawi ila hujakijua tu?

Mfano, mababu zetu zaidi ya maiak 100 iliyopita walivyoletewa gramophone inayopiga muziki bila mtu kuimba, waliona kama uchawi.

Lakini leo tunaelewa sayansi iliyotumika, tunaelewa si uchawi, ni sayansi tu.

Sasa wewe una hakika gani unachofikiri ni uchawi ni uchawi kweli na si kitu usichokielewa tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…