Ushawahi pata aibu gani mbele ya crush yako?

Walipita wanawake wawili mtaani ilikuwa usiku mvua inanyesha na mwamvuli nikamwambia mmoja mtu mzima na kisu shingoni ile namwangalia mwengine namsihi asikimbie wala asipige kelele kumbe crush


Alipigwa na butwaa
🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Walipita wanawake wawili mtaani ilikuwa usiku mvua inanyesha na mwamvuli nikamkaba shingoni mmoja mtu mzima na kisu shingoni ile namwangalia mwengine namsihi asikimbie wala asipige kelele kumbe crush


Alipigwa na butwaa
daaaa nimecheka mpka tumbo linauma
 
Nmecheka eti kuuza kuku.
 
Nilikuaga sina mchongo yaani sina kazi,

Huyo demu alikua anasoma form 3 na nilikua namsoteaga sana ila ndio hivyo alikua ananipuuzia sana,

Kwao nilikua napajua but nilikua sijawahi kufika wala kuingia mule ndani,

Sasa nilikua naishi na broo mmoja hivi yeye ndio alikua ananiunganishia Huyo mtoto,

Siku moja akaniambia kwamba dogo saivi inabidi tutafute kazi ya kufanya au unasemaje,

Mi nikamwambia fresh tu akasemema poa,

Nashangaa siku moja broo akaniijia na kuniambia dogo twende sehemu kuna mchongo naenda kuufatilia

Nikamwambia fresh tukaondoka mguu kwa mguu, nastuka hivi tunaingia mule ndani kwao Huyo demu,

Nikamwambia broo VIP tena humu mi sijawahi kuingia, akasema kuna mshikaji nampitia broo wake na Huyo demu unaesemaga wako, kwahyo we twende ndani,

Mwanzo niligoma kuingia ila alinilazimisha nikaingia,, broo akawasalimia nami pia nikamwona yule mtoto anashangaa shangaa tu,

Broo akaulizia kama jamaa yake kaja akaambiwa bado,
dakika 0 yule jamaa akaja wakaanza kuzungumza na broo,

Yule jamaa alikua anampenda sana mdogoake maana alipokua akiongea na broo na yule mtoto alikua pale pale, wakiongea ongea baada ya kupokeana na kukumbatiana,

Mara nikasikia jamaa yule akasema dogo mwenyewe ndio huyu?
Broo akajibu ndio huyu huyu,

Jamaa akaniuliza Eti dogo ushawahi kuchunga ng'ombe?

Mi nikashangaa ng'pmbeeee?

Broo akakazia kwamba huyu hashindwi maana sie tumekulia kwenye ufugaji,

Nikabaki nashangaa shangaa tu, jamaa akasema sie hapa tunazo ng'ombe 3 tu wa maziwa tena wa kizungu hawa hawachungwi Bali utakua unakata majani na kuyaleta humo zizini mwao,

Akaniuliza VP bei gani kwa mwezi?

Daaah nilibaki nashangaa tu, mwishoe nikainuka naondoka, broo akanikalisha chini tena na kuniambia tulia hapa dogo upate kazi acha ujinga wa kuruka ruka mtaani na viduku vyako unadhani ndio ujanja,?

Yule demu akawa anacheka kwa chini chini tu,

Daah nilibaki mpole tu maana broo mwenyewe sio haba ukimzingua anakuzingua kweli,

Aibu ya siku hiyo mpaka ntaingia kaburini aisee ,
broo nilimchukia mnooo, wala sikuwahi kumuuliza,

Ila aliwahi kusema kwamba nilikua namsumbua sana kuhusu Huyo demu,

Yaani nisipomwona basi nanyong'onyea siku nzima, na kila tukiongelea mademu mi namtaja Huyo huyo tu,

Kwahyo alifanya kunisaidia et kwa sababu zilikua zimepita kama wiki mbili sijamwona
 
daaah πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Pole sana πŸ˜›

Kwahiyo maisha yakaendeleaje baada ya hapo?
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] kavu sana huyo broh wako
 
Pole sana [emoji14]

Kwahiyo maisha yakaendeleaje baada ya hapo?
Baada ya hapo mtoto akawa ananitania kila nikikutana nae mweishoe ikawa mazoea,

Nikapita nae na mpaka sasa nipo nae hua namkumbusha hii kitu na kujisafisha pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…