Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Kuhusu masuala ya China, kwenye mkutano huo, G7 imeendelea na madai yake yaleyale yaliyotolewa mwaka jana kwenye mkutano wa Hiroshima nchini Japan, na kuipaka matope China katika masuala ya Taiwan, Bahari ya Mashariki, Bahari ya Kusini, Hong Kong, Xinjiang na Tibet. Mwaka huu, suala jipya linaloitwa “uwezo wa uzalishaji wa kupita kiasi” nchini China pia limetajwa. Kwenye taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, G7 imesisitiza haja ya kubainisha minyororo muhimu ya ugavi ndani ya kundi hilo, ikiilengea China ambayo ni injini kubwa zaidi ya uchumi wa dunia.
Kuhusu mgogoro kati ya Russia na Ukraine, G7 inaiunga mkono kwa nguvu zote Ukraine kuendelea na vita na Russia, lakini kwa upande mwingine, hailaani hata kidogo vitendo vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza ambavyo vinakiuka vibaya sheria za kimataifa. Aidha, kuhusu masuala haya mawili, Marekani na nchi wanachama wengine wa G7 pia zina mivutano mingi ya ndani, hali ambayo imeyafanya masuala hayo yawe magumu zaidi.
G7 ilianzishwa mwaka 1976, na wanachama wake ni pamoja na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Japan, Italia na Canada. Wakati huo, Pato la Taifa la Marekani lilichukua zaidi ya asilimia 29 ya uchumi wa dunia, kwa pamoja na Ujerumani na Japani, ambazo uchumi wao ulikuwa ukiendelea kwa kasi kubwa, kundi hilo liliwahi kudhibiti sehemu kubwa ya uchumi wa dunia, na kuwa nguvu muhimu ya kiuchumi duniani.
Ikiwa “Klabu ya Nchi Tajiri Zaidi Duniani”, G7 ingeweza kutoa mchango mkubwa katika kutatua matatizo ya kimataifa. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kundi hilo limeshindwa kuchukua hatua halisi za kukuza uchumi wa dunia, wala kuzisaidia nchi zinazoendelea kupata maendeleo. Ripoti iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Kutoa Misaada la Oxfam inakadiria kuwa, G7 imezikopesha nchi za Kusini takriban dola trilioni 13.3 za kimarekani, ikiwa ni pamoja na ahadi za misaada ya maendeleo na misaada ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa G7 imeshuka mwaka hadi mwaka, na umeshindwa na kundi la BRICS ukihesabiwa kwa bei ya ununuzi halisi. Licha ya hayo, hivi sasa mchango wa G7 kwa ukuaji wa uchumi wa dunia ni mdogo kuliko ule uliotolewa na China. Kundi hilo limegeuka kuwa chombo cha nchi za Magharibi kufanya umwamba.