The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga, imetenga fedha kiasi cha Sh.bilioni 1.3 kwa ajili ya kuwapatia wajasiriamali mikopo isiyokuwa na riba ili kukuza mitaji yao na kuondokana na mikopo umiza inayosababisha kuzikimbia familia zao.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Hadija Kabojela ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji na kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala.
Amesema, fedha hizo ni sehemu ya mapato ya ndani ya halmashauri na zitatolewa kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na zitawasaidia kukuza mitaji yao na kuondokana na mikopo umiza ambalo ni janga la Taifa.
Aidha Kabojela amesema, kati ya fedha hizo Sh. milioni 500 ni kwa ajili ya wanawake, milioni 300 vijana na milioni 100 ni kwa ajili ya wenye ulemavu na kuwasihi watakapozipata wahakikishe wanazitumia katika matumizi lengwa na kuzirejesha kwa wakati ili kuwapatia wajasiriamali wengine.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Rehema Edson, amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Mkoa wa Shinyanga umepanga kutoa zaidi ya Sh. bilioni 5, na hadi kufikia Februari mwaka huu zimetolewa zaidi ya Sh. bilioni 2 kwa vikundi vya Wanawake 119, Vijana 110 na vikundi 10 vya watu wenye ulemavu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha amewasihi wanawake na wasichana mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi na ujasiriamali zinazojitokeza ili kujiimarisha kiuchumi na kuacha kufanya biashara kwa mazoea.
Amesema,mikopo inayotolewa na halmashauri ikawe chachu ya kujiinua kiuchumi kwa kuzitumia katika matumizi yaliyopangwa nasio kwenda kununua mavazi mazuri na kuvaa badala ya kukuza mtaji, wale watakaoshindwa kuzirejesha watawajibishwa kwa mujibu wa serikali za serikali za mitaa.