Ushindani wa kibiashara: Fastjet yaja na aina mpya ya ndege "Embraer E190"

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kampuni ya ndege ya Fastjet kesho itaanza safari zake kwa kutumia ndege mpya aina ya Embraer E190 na kuwatoa hofu wateja wake kutokana na ubora wa ndege hizo.
Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kufafanua kuwa ndege hiyo itazunguka katika safari kama zile za awali.

"Kampuni imeporomoka kiuchumi, ni muhimu kuendana na hali ilivyo hatuwezi kuacha kuhudumia watu. Tumeleta ndege mpya na kesho itaanza kazi rasmi," amesema Corse.

Corse alisema ujio wa ndege mpya zilizonunuliwa na Serikali aina Bombadier wanaichukulia kama changamoto katika sekta ya usafirishaji wa anga pia ni maendeleo makubwa.
"Wafanye maendeleo zaidi, waingie maeneo ambayo hatufiki sisi kama Mpanda, Musoma ili kuwafikia watu wengi zaidi,"

Chanzo:Mwananchi

Bado naamini hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" makampuni matatu au zaidi ya ndege hapa nchini kwa safari za ndani.

Kama waliporomoka kiuchumi wakati ATCL hai-operate, leo hii wakianza kugawana abiria hali itakuwaje?

Mtafakari sana kwanini wanasema ATCL ifike kule ambako wao hawafiki(Mpanda,Musoma n.k).

Swali hapa ni je,sababu zinazowafanya wao wasifike huko haziwezi kuwafanya ATCL nao wasifike?Nani anapenda hasara?

Je,huu si mwanzo wa kubanana katika destination chache tu?

Unafikiri ni nini kitafuata hapo?

ATCL iwekeze zaidi katika safari za kimataifa kwa mtazamo wangu kama tunataka kufanikiwa.

Taarifa zaidi:

Kwa mujibu wa Channel habari za Biashara saa moja usiku huu,ndege hizi zina uwezo wa kubeba abiria 108 mpaka abiria 120.

Wameleta ndege 2 na ndege ya pili itawasili hivi karibuni.
 
Haya sasa atcl na fastjet tunaona nan ana huduma bora
 
technically
 

Ndege za fastjet haziwezi kutua kwenye viwanja vidogo ambavyo aina ya ndege za bombadier zinatua. Mara ngapi muambie hili?

Watanzania kwanini tunakuwa watu wa kukatishana tamaa? Kila kitu hakiwezekani hao wengine walioweza wana miguu kumi?
 
Mkuu umehitimisha vizuri sana ila hujatoa mapendekezo ya nini kifanyike ili kuleta huo ushindani unaotaka.
 
JF imeshuka sana

Hivi mpaka leo forum hii imeshindwa kuweka wazi majina ya vigogo serikalini na wallopo kwenye sect binafsi wanao ikwamisha fast Jet?
 
Ndege za fastjet haziwezi kutua kwenye viwanja vidogo ambavyo aina ya ndege za bombadier zinatua. Mara ngapi muambie hili?

Watanzania kwanini tunakuwa watu wa kukatishana tamaa? Kila kitu hakiwezekani hao wengine walioweza wana miguu kumi?
Huko Mpanda, ATCL itapata abiria wa kutosha ndugu yangu?

Tuwekeze katika safari za kimataifa angalau tunaweza kufanikiwa lakini sio kwa safari za ndani ya nchi.
 
Safari za kimataifa kwenda wapi mkuu?? Kila njia ina ushindani mkubwa tu! Labda tukomae safari za ndani kwanza tujue hata soko laendaje! Maana wamepewa wahandisi ambao hatujui uwezo wao kibiashara! Hatujui kama wameambiwa watoe huduma au biashara! Kuanza kwenda nje ni shughuli ingine mkuu!! Labd Hayaya.....pekee
Huko Mpanda, ATCL itapata abiria wa kutosha ndugu yangu?

Tuwekeze katika safari za kimataifa angalau tunaweza kufanikiwa lakini sio kwa safari za ndani ya nchi.
 
...
.....vitwangarizimu visikosekane na mitanda ....Sauziafrika eyabasi
 
Ndege za fastjet haziwezi kutua kwenye viwanja vidogo ambavyo aina ya ndege za bombadier zinatua. Mara ngapi muambie hili?

Watanzania kwanini tunakuwa watu wa kukatishana tamaa? Kila kitu hakiwezekani hao wengine walioweza wana miguu kumi?

Nani kakudanganya? Wanaleta ndege ambazo zitakidhi mahitaji ya watanzania.
Na wako kibiashara zaidi sio magumashi kama ATCL
 
AIR TANZANIA Wameanza na round trip 380,000 ...nina uhakika kings of Budget fares ...kwakuwa wamepata challange wanakuja na ndege za 200,000 round trip .......sina shaka na hilo
 
serikali kuingia biashara ya ndege wajipange kweli .....hizi kampuni binafsi kwa kubana matumizi ndio wenyewe sasa ....wewe fikiria kuna kampuni inaitwa FLYDubai Wao nao wamekuja na ndege za nafuu kati ya DAR -DUBAI ...Wanagonga round trip usd 360 hadi 400 against upper market EMIRATES ambao wao wanatoza usd 680 hadi 800 round
FLYDubai pia inamilikiwa na emirates kama wanahisa lakini target ni soko la economy ..zaidi
 
JF imeshuka sana

Hivi mpaka leo forum hii imeshindwa kuweka wazi majina ya vigogo serikalini na wallopo kwenye sect binafsi wanao ikwamisha fast Jet?
Wewe kama mwana JF kwanini usiokoe jahazi kwa kutuwekea hayo majina ya vigogo wanaokwamisha fastjet?
Maana hadi unasema hivi yapo unayoyajua.
Wengine nami nikiwemo hatuna habari kama kuna jambo la aina hiyo.
 
Huko Mpanda, ATCL itapata abiria wa kutosha ndugu yangu?

Tuwekeze katika safari za kimataifa angalau tunaweza kufanikiwa lakini sio kwa safari za ndani ya nchi.
Safari za kimataifa zahitaji ndege kubwa,ndiomaana mabasi ya coaster yanafanya safari fupi na scania safari ndefu
 
Soon Precision nao watakuja na ndege mpya.

air Tanzania wamenunua ndege mpya ....Hawa Precision walishawahi kumiliki hadi ndege 20 ATR na kuna wakati ilikuwa ndio shirika pekee linalotufunika uchi ....bila precision KENYA airways wangetuonea sana ..
Walikuwa wanaenda vizuri hadi pale Kenya airways walipofanya mbinu chafu ya kuinunu ....hili ilitakiwa idara ya usalama igundue ......walinunua Precision halafu wakaanza kufanya mbinu chafu za kuiuwa ..
walichofanya walinunua hisa 51% za mzee Michael Shirima ....lakini baada ya kununua hawakuweka mtaji walioahidi na wakaanza kuhujumu route za Precison ...pia wakimtumia Meneja Mkenya Michael Kioko ..wakaingiza Precision kwenye mkataba wa kununua ndege 10 mpya toka ATR huku wakijuwa mtaji walioahidi hawajaweka ......
Mzee wa watu akaja kushituka too late ...akamuondoa meneja mgeni akamuweka meneja mzawa ......tena mwanamke ambaye amejtahidi sana kufukia hasara .....na naona karibuni nao wanakuwa vizuri ....

Ilibidi mzee shirima kuangukia kwa Wakenya kupata mtaji zaidi baada ya kuwa ombi lake la kupewa mkopo nafuu na serikali kukataliwa kwa sababu za kibinafsi na chuki tu .hata alipoamua kuuza share zingine Nairobi na Dar stock exchange ...watu hao hao wabaya wenye chuki kwa mzawa waliandika barua kwenye mashirika yaliotaka kununua hisa hasa ya hifadhi kuyakataza yasifanye hivyo ....hili nilisikia mwenyewe kwa masikio Mwenyekiti mmoja wa bodi za haya mashirika akiwa VIP lounge akimuambia mkubwa mmoja kuwa walipewa maelekezo mahsusi ya kutonunua hisa za precision ili kumkomoa Mzee Shirima .... , alikuwa anastahili mkopo kwakuwa alikuwa anasaidia sana serikali upande wa kubeba watalii ....na alistahili kukopa hakutaka bure ....au hata wangemdhamini ....huyu mzee anastahili tuzo kwa kuweza kusimama tena Kenya Airways tayari walikuwa wamemmaliza.
 
Kilichobaki kwa ATCL ni mkakati wa kibiashara, na wafanyakazi wenye uweledi wa taaluma zao hata kama wanatoka nje ya nchi. Mdogo mdogo na sisi tunajifunza.
 
Labda fastjet waweke fixed price ya tiketi zao hii mambo ya kusema wana tiketi hadi za elfu 60 kwenda mwanza alafu ukienda kukata unakuta tiket laki 4,,,watasubiri sana kwa ATCL...!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…