Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Kama unafuatilia uchaguzi unaoendelea nchini Marekani basi bila shaka utakuwa umemuona Bilionea Elon akiwa bega kwa bega na Donald ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa 47 wa Marekani.
Ikumbukwe kuwa Elon wakati wa uchaguzi ametumia akaunti yake ya X pamoja na ushawishi wake wa kifedha kushawishi wananchi kumuunga mkono na kumpigia kura Trump.
Nimewaza kwa mfano kwa hapa Tanzania mtu kama Mo au Bakhressa apate kitengo serikalini. Hiyo si inamaanisha kuwa kuna namna wangeweza kutumia ushawawishi wao kunufaisha biashara zao?
Scholars na wabobezi wengi wa siasa za Marekani wamedokeza kuwa ushindi wa Trump utaenda kumsaidia Musk kwenye shughuli zake.
Soma pia: Elon Musk awa kivutio kwenye kampeni za Trump, aonekana akishangilia jukwaani
Haya ni baadhi ya manufaa atakayoyapata Musk baada ya Trump kushinda:

- Ushawishi wa Moja kwa Moja Serikalini: Serikali ya Trump inaweza kumpa Musk nafasi ya ushawishi wa moja kwa moja serikalini hivyo kuwezesha biashara zake kama Tesla, SpaceX, The Boring Company, Neuralink, na X kufaidika moja kwa moja kupitia utaratibu wa vibali, kanuni, ruzuku, na mikataba ya serikali.
- Mazingira Huru ya Udhibiti na Punguzo la Kodi: Trump ameahidi kupunguza kanuni za udhibiti wa biashara na kodi kwa makampuni na watu binafsi. Hii inaweza kupunguza vikwazo kwa biashara za Musk na kuongeza faida.
- Uhuru Zaidi kwa Teknolojia: Erik Gordon, kutoka Chuo Kikuu cha Michigan, alisema kuwa, chini ya Trump, Musk ataweza kuwa na uhuru zaidi wa kukuza teknolojia za kisasa hasa teknolojia kama Self Driving Cars na nyinginezo. Sasa itakuwa ni rahisi kwa Musk kupata vibali kwa kampuni yake ya Tesla kupeleka magari barabarani hasa katika majimbo ya Texas na California
- Fursa Kubwa za Mikataba ya Kijeshi kwa SpaceX Francesco Trebbi, profesa wa biashara katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley, alieleza kuwa Trump anaweza kusaidia SpaceX kupata mikataba mikubwa na Wizara ya Ulinzi na hivyo kusababisha Musk kupata tenda zaidi ya washindani wake kama Blue Origin.