Umutimbaru
Member
- Jul 22, 2011
- 91
- 5
Maonyesho ya Nanenane ni maonyesho ambayo wakulima huwa wanonyesha mzao yao. Wataalamu wa zana mbalimbali na wafanya biashara kuonyesha zana zitumikazo kurahisishia wakulima hao kupata mazao yaliobora kwa gharama ndogo. Wana JF shida yangu ni namna gani hawa wanaoandaa maonyesho haya na nivigezo gani wanavyovitumia katika kuchaguwa washindi. Ni wakulima gani wagani wanaoshindanishwa. Na mshindi anapopatikana huwa Anakuwa amefundisha nini jamii ya wakulima ambao niwengi wenye uwezo wao ni mdogo na wakati.Mwaka Fulani nilitembelea kiwanja kimoja cha maonyesho na ilikuwa ni siku ya kutangaza Mshindi wa maonyesho ya kilimo cha bustani na kweli aliechaguliwa bustani yake ilipendeza ilikuwa nzuri sana kuliko zote katika uwanja huo, kwani mchicha ilipendeza sana sukuma wiki ilipendeza sana na mazao yote yalioandaliwa yalikuwa mazuri sana yalivutia.Shida ya hawa wanao pima matokeo haya wanazingatia gharama ya kuzalisha hayo mazao. Mkulima wakawaida baada ya kuona mazao haya anafaidika nini? au anajifunza nini?.Kwa mawazo yangu hawa wanaotadhimini ushindi wa hao wataalamu wangelikuwa wanalenga ni njia ipi mkulima wakawaida anaweze kulima kwakuzingati hali halisi ya eneo, upatikanaji wa mahitajio mfano maji, mbolea, mbegu bora na vinginevyo na kupata mazao Kama yao. Likini unakuta Mshindi anatumia gharama kubwa ambayo hata hailingani na zao Hilo likiuzwa katika soko la kawaida.Wana JF Mnaonaje hilo wazo.