Ushindi wa simba sc msimu wa 2021 unatoa picha ya ubora na ubovu wa vilabu vyetu

Ushindi wa simba sc msimu wa 2021 unatoa picha ya ubora na ubovu wa vilabu vyetu

Ladder 49

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
7,918
Reaction score
20,037
Wakuu Habari zenu?

Nikianzia mechi ya juzi ya mtibwa na simba ambayo mtibwa alikufa 5 bila.

Ukiangalia namna simba alivyocheza na mtibwa utagundua vilabu vyetu bado havina huwezo wa kushindana kimataifa isipo kuwa simba peke yake.

Timu tofauti na simba haiwezi kupiga pasi kufikia kumi (hapo nimezidisha sana hiyo idadi )sasa kama ndio hivyo hayo magoli utafungaje?

Mechi ya simba na mtibwa kuna muda Nilikuwa naona mtibwa wanaanzia nyuma mpira ,kipa anaanzisha nyuma lakini hawafikishi pasi kumi wanakuwa huo mpira wameshawapa simba,sio simba kuwakaba wenyewe wanakuwa wanaupoteza.

Na Kuna muda mwingine pia wanakuwa wanaweka mpira chini wapige pasi washindane na simba,nikawa nacheka mwenyewe maana Hapo kwa mkapa al ahly mwenyewe kashindwa kupiga pasi utakuja kuweza wewe mtibwa? Nikaona wanatimiza wajibu tu kwamba walicheza na simba tu basi,ila wanachokifanya uwanjani hakuna kitu yaani hakiwezi kuwatisha simba wakaondoka na point 3.

Kwa sasa mechi za simba dhidi ya timu yoyote ile itatoa picha ya vilabu vingine kuonekana mazoezini
wanakuwaga wanapanga koni tu maana hivyo vilabu haviwezi kupiga pasi kumi wanaishiaga pasi 6 tu mpira wanapoteza.

Kwa sasa timu zetu ukindoa simba zinatakiwa kuiga kwa simba ,ule mpira wa kurusha ndege(kubutua mbele tu) umepitwa Na wakati .mpira kwa sasa unanjia zake(mpira ni science) kwa simba inavyocheza itaendelea kutawala soka la bongo mpaka wenyewe waseme basi.

Kwa sasa simba anavyocheza hakuna mechi ngumu kwake kwa sababu anafata njia za mpira unatakiwa uchezejwe? Na hakuna timu inayocheza mpira wa kueleweka mpaka kwenda kufunga .simba inacheza kama man city,ana cheza kama Psg ,anacheza kama liverpool,anacheza kama Real Madrid anacheza kama timu zingine za ulaya,wakati timu zingine zimebaki na kupanga koni kwenye mazoezi na kwenye mechi kupiga mpira mbele tu,

timu zingine tofauti na simba haziwezi kukaa na mpira wala kupiga hata pasi 7 tu haiwezi.sasa hizo timu zikicheza na simba zinatoa picha na kudhiirisha ubovu wa timu zetu tofauti na simba timu zetu za kwenye ligi yetu haziwezi kufika mbali kimataifa.mpaka zibadilike.

Ni hayo tu Wakuu.
 
Hawatakuelewa wenye timu zao(yao), wanahisi unajipendelea ila mioyoni wakikiri usemayo kuwa ni ukweli mtupu
 
Simba hii hii ya mo iwe sawa na man city? Livapuul,? Acha utani boss. Ngoja uone bao atakazokula kwa mc alger au benzohuldad nikuone kama utaisifia tena

Mkuu umekariri maisha wewe,hizo kauli zilikuwaga zamani.hata mimi ukiniambia siwezi kuamini lakini ndio ukweli huo simba imebadilika inazidiwa na ubora wa wachezaji tu ila namna inavyocheza huwezi kutofautisha na timu za ulaya.

Wewe endelea kukariri,hata sasa simba ndio club iliyomfunga club bingwa duniani namba tatu,kauli kama hiyo utadharua kwakua ufatilii umebaki na akili yako ya zamani.maana ni kitu ambacho akiwezekani

Simba anacheza mpira ambao unaonekana hadharani sio tu kupiga bu! bu !.
 
Basi itakuwa kazi ya Didier Gomez da Rosa. Huyu kocha anaonekana ni fundi kweli kweli. Kishingo asingeweza hayo unayosema
 
Dah ni kwel kabisa muda mwingne huwa nawaza iv vilab vingine wanashindwaje kupamban uwanjan wakat nao n wachezaj wanapiga matiz kama simba lakn wakishafika uwanjan amn la maana japo simba ni chama langu huwa napenda kuangalia mpira wenye ushindan siyo kuchukua point kizembe
 
Kucheza siyo tatizo kule wao simba kufungwa bao sita na sevilla ndiyo shida ilipoanzia
hizo sita walicheza lini

1618591994066.png
 
Dah ni kwel kabisa muda mwingne huwa nawaza iv vilab vingine wanashindwaje kupamban uwanjan wakat nao n wachezaj wanapiga matiz kama simba lakn wakishafika uwanjan amn la maana japo simba ni chama langu huwa napenda kuangalia mpira wenye ushindan siyo kuchukua point kizembe

Kila mechi ya simba . Mashabiki hawana pressure yoyote kwenye kila mechi lazima wafunge goli.
 
Mpira wa Simba walioonyesha dhidi ya Mtibwa umewazibua wanayanga ambao siku zote waliaminishwa kuwa timu yao inapoteza matokeo kutokana na hujuma, sasa hivi wamekaa na kukubali wachezaji wao wanaosajili kwa bei ndogo hawana uwezo wa kushindana na Simba badala yake inabidi watafute wachezaji wenye uwezo na kuwekeza nguvu kubwa zaidi ili kupata matokeo bora.
Hii imedhiirisha kwa vitendo Simba ni next level maana wao wanaanza wengine wanaiga.
 
Bado sijawakubali simba,kwangu naona ni kama wacheza mazingaombwe tu
Mbaya zaidi kuturogea timu yetu isipate ushindi na kuwafunga washambuliaji wetu kichawi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom