Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Wakuu, kama mnavyojua, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanya chaguzi mbalimbali kuanzia ngazi ya Kanda hadi Taifa. Jambo moja lililonivutia kufikiria kwa kina ni ushiriki mdogo wa wanawake katika nafasi za uongozi. Hili ni tatizo linalozidi kuathiri usawa wa kijinsia katika siasa zetu, jambo ambalo linapaswa kujadiliwa na kutafutiwa suluhisho.
Niachane na ngazi ya kanda ambako ni fezea tupu, hali hiyo inaonekana kwa mabaraza ya vyama. Ukiondoa BAWACHA, ambalo kimsingi limeundwa kwa ajili ya wanawake pekee, mabaraza mengine kama BAVICHA na BAZECHA yanaonyesha uwakilishi wa wanawake wa kiwango cha chini mno.
Kupata taarifa na matukio kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hii inadhihirika pia kwenye uchaguzi wa jumla wa viongozi wa ngazi za juu, ambapo asilimia 99.9 ya wagombea ni wanaume. Hali hii si tu inaminya fursa kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika maamuzi, bali pia inakwamisha juhudi za kufikia usawa wa kijinsia ambao ni sehemu muhimu ya maendeleo ya kidemokrasia.
Soma Pia kwa taarifa zaidi zinazowahusu wanawake kipindi hichi cha uchaguzi: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?
Wakuu, mnadhani nini shida hasa? Na nini kifanyike kupunguza gap hili baina ya wanaume na wanawake?