Pre GE2025 Ushiriki wa vijana wa kike kwenye uchaguzi nchini ni suala muhimu katika kuimarisha demokrasia

Pre GE2025 Ushiriki wa vijana wa kike kwenye uchaguzi nchini ni suala muhimu katika kuimarisha demokrasia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Ushiriki wa vijana wa kike kwenye uchaguzi nchini Tanzania ni suala muhimu katika kuimarisha demokrasia na kuhakikisha uwakilishi sawa. Vijana wa kike wanakumbwa na changamoto nyingi, kama vile ukosefu wa uelewa wa haki zao za kisiasa, kukosa fursa za kushiriki kikamilifu kwenye kampeni au michakato ya uchaguzi, na vikwazo vya kijamii au kiuchumi.

Katika miaka hii miwili Nchini kwetu kutafanyika uchaguzi kwa mwaka 2024 uchaguzi wa serikali za mtaa na mwaka 2025 utafanyika uchaguzi mkuu. Nimejaribu kufuatilia kuanzia kujiandikisha kwenye daftari la mkazi kwajili ya uchaguzi wa serikali za mtaa maeneo mengi muamko wa vijana wa kike umekuwa si mkubwa kwenda kujiandikisha.

Lakini pia kumeanza kupigwa kura za maoni kwenye vyama vya kisiasa mfano CCM lakini waliodhubutu kuchukua fomu kwa kweli ni huzuni sana yani idadi yake ni ndogo sana.

Nimejaribu kutazama nini kinasababisha ushiriki wa vijana wa kike kushindwa kuingia kwenye siasa

Kukabiliana na vikwazo vya kijamii- Wamekuwa awaaminiki na kuonekana kama awawezi kuongoza kabisa lakini mimi naamini uwezo wanao na ukizingatia kwa sasa vijana wengi wa kike wamesoma na wanaelimu zao nzuri tu kwahiyo wakipata nafasi wanaweza kuleta chachu ya maendeleo.

Uchumi- Hii pia ni moja ya changamoto inayowakumba sana kundi kubwa na vijana wa kike hata wanawake katika kushiriki na kuwania nafasi za uongozi wakizani kuwa na uchumi mkubwa ndiyo kupata nafasi ya uongozi lakini ni jambo ambalo si la kweli. Bali uongozi ni kujitoa na kuwatumikia kwa uweledi kwa wale unaowaongoza.

Elimu ya uraia – Vijana wa kike wanapaswa kufundishwa juu ya haki zao za kupiga kura na umuhimu wa ushiriki wao kwenye siasa.

Kikubwa Vijana wa Kike msiogope kujitokeza kwenye siasa fanyeni kweli mnauwezo lakini tumieni elimu zenu kuweza kuleta mabadiliko chana kwenye uongozi na kuwakomboa wanawake wengine ambao wapo kwenye changamoto.

Inawezekana hakuna mtu aliyeamini kuwa kuna siku Tanzania itapata Rais mwanamke kama sasa Rais wa Tanzania ni Samia Suluhu lakini si yeye pia hata Spika wa Bunge ni Mwanamke ambaye ni Tulia Ackson
ambaye pia ni Rais wa Mabunge Dunia (IPU) na wengine wengi tu ambao wanaweza kuwa mifano lakini chachu nzuri kwa vijana wa kike katika kushiriki vyema kwenye siasa hadi kufikia uongozi.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Tufanye nini ili kuongeza ushiriki wa wanawake hasa vijana kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
 
Back
Top Bottom