BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Ushirikiano na Kenya usiangalie kingine ila maslahi ya Tanzania.
Rais Samia Suluhu Hassan ameitembelea Kenya katika ziara inayoelezwa kuwa imefungua ukurasa mpya wa mtangamano unaoashiria kuimarisha udugu na ujirani baina ya mataifa hayo.
Akiwa Nairobi anahutubia wafanyabiashara na wabunge wa bunge la kitaifa na la seneti wote akiwahakikishia kuwa anatamani kuona uhusiano endelevu kati ya Kenya na Tanzania.
Anawaambia wabunge:
"Binafsi nashangazwa sana na wale wanaodhani Kenya na Tanzania ni wapinzani. Mbaya zaidi ni kule kuamini kwao kwamba hilo linawezekana tu mmoja wetu kumwangusha mwenzake. Hawa ni watu wenye mioyo ya choyo, maono mafupi na akili mbovu."
"Ni bahati mbaya kuwa wapo katika pande zote mbili, Kenya na Tanzania. Hutokea pia wachache wao wakawa ni watumishi wa serikali na hata wanasiasa wa pande mbili…"
Aidha, Rais anaahidi kuwa awamu ya sita itahakikisha kuwa Kenya inabaki kuwa ndugu, jirani na mshirika wa mkakati, ahadi ambayo baadhi ya wadau wanaisifu na kuona kuwa ni mwanzo wa kudumisha ushirikiano, lakini ni lazima ulenge kwenye maslahi ya Watanzania na zaidi ya hapo utakuwa hauna tija.
Akizungumza na Nipashe kuhusu hotuba na ziara ya Rais Nairobi, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Katiba Tanzania, (JUKATA) Bob Wangwe, anakumbusha haya:
“Jambo la muhimu pamoja na udugu na ujirani wetu na Kenya lolote lazima liwe ni maslahi ya Watanzania. Hiki ndicho kiwe kipaumbele katika kila uamuzi tunaochukua kama nchi.”
Anaunga mkono ziara ya Rais Samia, akisema ni muhimu kwani itazisaidia nchi zote mbili kujenga uelewano ambao ni muhimu katika maendeleo ya mataifa hayo kwani Kenya na Tanzania zinategemeana.
Hata hivyo, anapoulizwa kuhusu hofu kuwa mara nyingi ushirikiano umekuwa na wasiwasi, anasema hofu hazikosekani ni lazima ziwepo kwani kila nchi inafikiria zaidi kutumia fursa inazopata kwa ajili ya kuendeleza mipango na mikakati yake, hivyo kipaumbele cha kuwanufaisha Watanzania ndicho kiwe suala la msingi.
Anakumbusha kuwa ili kuwa na uhusiano na ushirikiano wenye tija kwa pande zote mbili au ‘win win situation’ ni vyema serikali mbili zingine kwenye makubaliano kwa kutambua na kuzingatia tofauti baina zao.
Anapoulizwa kuhusu suala la baadhi ya Watanzania kuona kuwa kuna mambo yanayofanywa na majirani zao ambayo yanakwenda tofauti na mustakabali wa taifa lao, mfano kutangaza Mlima Kilimanjaro kuwa uko nchi jirani.
Aidha, mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa soko kuu la bidhaa za Tanzania kinyume cha utaratibu Wangwe anasema.
“Inapotokea nchi inavunja makubaliano ya pamoja ya jumuiya hiyo ni jukumu kwa jumuiya kuwajibika katika kulinda misingi na makubaliano ya pamoja. Siyo vyema kutupiana lawama.”
Mkurugenzi Mtendaji wa JUKATA, anahimiza kuendelea kukuza uelewano wenye tija baina ya nchi wanachama na hili ndilo litakaloleta utashi wa pamoja katika kuheshimu misingi wanachama waliojiwekea.
KUTAZAMA TOFAUTI
Wangwe akizungumzia ahadi za Kenya kwa Watanzania mfano Rais Uhuru Kenyatta, anaahidi kwamba nchi yake iko tayari kuwapokea Watanzania kuendesha shughuli zao bila vibali vya ukazi na kazi.
Anafafanua kuwa kwa Kenya ni sawa lakini Tanzania ikiruhusu hilo itakuwa imefanya kosa kubwa kwa kuwa bado watu wake hawajaandaliwa.
“Hii itakuwa sahihi kama tukifanya hivyo kwa wawekezaji hasa wa daraja “A”. Tanzania tuna ardhi kubwa kweli, lakini ni kwa ajili ya Watanzania. Leo tukibadilisha mifumo yetu ya kisheria kwa lengo la “kuhonga” ardhi yetu kwa msamiati wa udugu na ujirani tutakuwa tumewakosea sana wajukuu zetu na wazee wetu ambao walitulindia ardhi hiyo.”
Anaeleza kuwa ni muhimu kushirikiana lakini maslahi ya Watanzania yawe ndicho kipaumbele bila kujali kingine na mipango ifanyike kwa kuangalia tofauti zilizopo baina ya washirika.
Rais anaahidi kuboresha na kuondoa vikwazo vya biashara vilivyopo Tanzania vinavyoathiri ushirikiano kati ya wafanyabiashara wa mataifa hayo akiahidi kuvishughulikia na ili kuwepo na biashara isiyo na vikwazo, lengo liwe ushirikiano unaoleta tija.
Wangwe anazidi kukumbusha kuwa katika hatua yoyote lazima suala la tofauti ya nchi zote mbili lizingatiwe ili mataifa yote yanufaike.
“Ni bahati mbaya sana kwamba hatua zetu Watanzania kama nchi bado ni chache ukilinganisha na Kenya, hivyo lazima tushirikiane kwa kutambua hili.”
MAONI YA WADAU
Mmoja wa wakulima wanaozungumzia biashara baina ya Kenya na Tanzania anaomba serikali itazame sheria za kununua mazao mabichi mashambani.
Wakulima Arnold Mkupete na Kulaga Ngomale, wanasema wanalima maeneo ya Mvuha na kijiji chao kinazungukwa na maji ya Mto Mvuha na mara nyingi wanafikiwa na wakulima kutoka nchi jirani ambao wananunua mazao mashambani tena kwa bei kiduchu.
Mkupete anasema: “Kuna maeneo ambayo yanawaumiza wakulima ni wageni wanaofika vijijini kununua mazao mabichi. Kwa mfano wananunua iliki mbichi kwa bei ndogo sana. Tunaomba hili likaangaliwe.”
Anaungwa mkono na Kulaga anayeshauri kuwa kuwe na magulio vijijini kama yalivyo kwenye kuuza na kununua korosho, ufuta na pamba na serikali itoe bei elekezi ili wakulima wafaidike badala ya kuacha mambo yabaki kama yalivyo ambayo hayana tija.
Baadhi ya wakulima wengine wanaozungumzia biashara za mashambani ni wa kutoka Kilimanjaro na Arusha wanaosema wafanyabiashara majirani wananunua maparachichi, mbaazi, vitunguu na mazao mengi kwa bei ndogo na kutaka kuwe na utaratibu mpya wenye tija mbali na kutaka magulio.
Wanashauri kuwe na utaratibu wa kutaja asili ya bidhaa (place of origin) na serikali kusaidia wakulima na Watanzania kupata soko la bidhaa nje moja kwa moja badala ya kuachia wageni wanaozinunua na kuziuza ughaibuni kwa faida kubwa kama za wakati walizinunua vijijini kwa bei kiduchu.
SOURCE: NIPASHE