Ushirikiano wa kunufaisha kati ya China na Afrika ni endelevu

Ushirikiano wa kunufaisha kati ya China na Afrika ni endelevu

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
1736404781899.png


Miezi machache baada ya mkutano wa kilele wa Beijing wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC kufanyika mwaka jana, wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wamekuwa wakifuatulia maendeleo ya utaratibu wa FOCAC na mchango wake kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika, hasa kama utaratibu huo umekuwa na manufaa kwa China, nchi za Afrika na kwa watu wa pande hizo mbili. Kwa ujumla uchambuzi mwingi umeonesha kuwa utaratibu huo umekuwa na matokeo mazuri.

Moja ya mambo yanayotajwa zaidi kuhusu utaratibu wa FOCAC, ni kuwa umeweza kuzipatia nchi za Afrika na watu wake fursa ya kutumia uwezo wa ndani kujiendeleza, na kutumia mahusiano ya kidiplomasia na China kuchochea maendeleo ya kiuchumi ya nchi zao. Hii ni tofauti kabisa na ambacho kimekuwa kinatajwa na nchi za magharibi kwa muda mrefu, kwamba bara la Afrika ni bara linalotegemea misaada kutoka kwa nchi za magharibi na haliwezi kujitegemea.

Pamoja na ukweli kwamba nchi nyingi za Afrika bado ziko nyuma kiuchumi, juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na nchi hizo zimekuwa zikikwamishwa na mfumo wa uchumi wa dunia unaodhibitiwa na nchi za magharibi. Mfumo ambao unazifanya nchi za Afrika kuwa ni vyanzo vya bei rahisi vya malighafi na masoko ya bidhaa za viwanda vya nchi za magharibi. Kuibuka kwa China kwenye jukwaa la uchumi duniani na kuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi na ukaribu wake na nchi nyingi za Afrika, kumekuwa kunabadilisha hali hiyo na kuwa na matokeo chanya.

Utaratibu wa FOCAC na taratibu nyingine za upande mmoja za China (unilateral steps), zimefungua soko la China kwa nchi za Afrika na kuweka hatua nyingine mbalimbali za kuchochea uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika. Kwa sasa kuna maonyesho ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa ya China (CIIE), na kuna maonesho ya kilimo ya Changsha, ambayo yanahimiza nchi za Afrika kuingiza bidhaa nchini China.

Kwa mkulima au mfanyabiashara wa kawaida wa Afrika, ufinyu wa soko kimekuwa ni kilio kikubwa kwa muda mrefu. Nchi za Ulaya na Marekani zimekuwa ni washirika wa jadi wa kibiashara na nchi za Afrika. Kupata nafasi ya soko la Ulaya au Marekani, ni sawa na ndogo ya alinacha. Marekani kupitia mpango wake wa AGOA, na Umoja wa Ulaya kupitia mpango wake wa ACP, wamekuwa na masharti mengi na magumu kwa nchi za Afrika, masharti ambayo yanalenga bidhaa fulani au nchi fulani, na pia yanalenga kuimarisha masoko ya bidhaa za wazalishaji katika nchi zao.

Mara nyingi tumekuwa tunasikia China inainua ushirikiano wake na nchi mbalimbali za Afrika na kuwa “ushirikiano wa kimkakati wa pande zote”. Hatua hii ni hatua ya uhakikisho wa ushirikiano wa kunufaishana. China imepiga hatua ya maendeleo kwenye kila nyanja, iwe ni elimu, sayansi, teknolojia, uchumi, nk, na nchi za Afrika zina mahitaji mengi kwenye maeneo hayo. Utaratibu wa sasa wa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika unagusa maeneo yote, ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo nchi za Afrika zinahitaji misaada kutoka nje, na hata maeneo ambayo nchi za Afrika zinaweza

Baadhi ya wachambuzi wa nchi za magharibi wamekuwa wakiutazama ushirikiano kati ya China na Afrika kama ni tishio kwao, kwa maana ya kuwa unaingilia himaya yao. Lakini kwa nchi za Afrika, ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika ni ushirikiano endelevu, kwani kupitia mipango inayogusa sekta mbalimbali na inayonufaisha pande mbili, iwe ni ngazi ya serikali, mashirika na hata watu binafsi, inakuwa inajenga msingi mpana wa ushirikiano endelevu, wa kuaminika na wa kuzinufaisha zaidi nchi za Afrika.
 
Back
Top Bottom