Ushirikina (chuma ulete) unawaangusha wafanyabiashara

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2011
Posts
3,402
Reaction score
925
Wasalaaam!

Ni po kwa masikitiko juu ya aina hii ya uchaw kwenye biashara,nakumbuka siku moja jamaangu mmoja anafanya biashara ya duka la madawa na M-Pesa alikutwa na msala wa kupoteza laki nne katika mazingira tatanishi.

Alikuja binti akiwa ma mama wa makamu wakiwa na elfu kumi wakanunua dawa za elfu mbili na kupewa chenji elfu nane, jamaa kachukua ile elfu kumi akachanganya na milion mbili za m-pesa, baada ya dk tano kaja mtu anataka kutoa laki tano kwenye m-pesa, jamaa kucheki tayari ana loss ya laki nne!

Najaribu kufikilia dawa hasa ya huu mchezo wa chuma ulete nini?

Kaka'angu ana ofisi ya stationery, haya yanamkuta kila mara, alishawahi kushauriwa na wenzake kwamba akimstukia mtu kama atahitaji huduma ambayo itahitaji chenji basi ni kumwambia chenji baadae, then akiondoka anaenda kuchenji sehemu nyingine, bila hivyo hesabu maumivu.

Dawa hii ya chuma ulete itakomeshwa vipi? Isiwe kwa mganga.
 
Imani yako ndio kinga yako. Hakuna dawa kubwa kama imani inayopelekea wewe kujiamini. Kuna njia nyingi za kuongezea nguvu katika imani, mfano kutumia biblia au Quran.
 
Si amini kama kuna uchawi bali ni "illusion".Kuna watu wanaamini uchawi mpaka wanafikia point wana "hallucinate".If your bro and friend are not one of them,can install cctv systems na watawona wachawi wa kweli
 
Mwambie aje tabora nimpeleke kwa mtaalam.
Amini usiamin hiyo technology ipo,na ulinzi pia upo....jaribu kuwaona watu wanaouza sokoni,wanajua wapi wanatoa ant-chuma ulete.
 
Kuna mama wa kichina alishanifanyia huu mchezo mara mbili, kuna siku nilienda kwake nikamlipa hela yake niliporudi nyumbani nikakuta $25 zimeyeyuka mifuko ya suruali haijatoboka hela zingine zipo nikajipa moyo nimeidondosha, siku nyingine nikaenda tena kwa yule mama kupata huduma nilporudi nyumbani $25 tena hazipo hela nyingine mfukoni zipo.... ndio nikagundua mchezo wa mama wa kichina.

Haya madudu yapo jamani, wewe angalia process ya muhindi anapokupa hela it's whether anakupa kwa mkono wa kushoto au anaweka mezani sijui ndio anti-chumaulete![hawa jamaa huwa ni wachafu sana]
 
kwani hawa chuma ulete hawaibi ebay, itunes, kwenye giants companies.... Solution ni kwamba they are fake
 
do pole sana mkuu,lakini watu wanakataa et hamna kitu cha hivyo nafikili haijawatokea
 
Mwambie aje tabora nimpeleke kwa mtaalam.
Amini usiamin hiyo technology ipo,na ulinzi pia upo....jaribu kuwaona watu wanaouza sokoni,wanajua wapi wanatoa ant-chuma ulete.
mkuu wengine tunaogopa waganga itakuje?
 
Si amini kama kuna uchawi bali ni “illusion”.Kuna watu wanaamini uchawi mpaka wanafikia point wana “hallucinate”.If your bro and friend are not one of them,can install cctv systems na watawona wachawi wa kweli
mkuu amini usiamini uchawi upo na hata vitabu vya dini vimeeleza kuwa uchawi upo
mkuu sikuombei ikutokee lakini kama ni mfanya biashara mdomdogo utakua tayali umeshakumbana nayo au itakupata tu
 
mkuu amini usiamini uchawi upo na hata vitabu vya dini vimeeleza kuwa uchawi upo
mkuu sikuombei ikutokee lakini kama ni mfanya biashara mdomdogo utakua tayali umeshakumbana nayo au itakupata tu
Kitabu gani nani sehemu gani katika kitabu wame acknowledge existance of witchcraft?
 
Kitabu gani nani sehemu gani katika kitabu wame acknowledge existance of witchcraft?

Biblia inasema Musa alishindana na wachawi walioletwa na Farao,
Biblia inasema usimwache mwanamke mchawi akaishi. Unataka na aya mkuu?
 
aka katabia kakujipatia fedha kirahisi tu kwa ushirikina kananikera kwerikweri
 

mi mwenyewe yalishanikuta tena kwa omba omba wa barabarani. Ingawa sikuliwa hela nyingi ila ilinifanya niprove kuwa haya mambo kweli yapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…