Ushirikina Migahawani

Ushirikina Migahawani

SAINT MATATA

Member
Joined
Dec 5, 2022
Posts
21
Reaction score
34
Leo ni wikiendi na kwa kiasi kikubwa upande wangu mishemishe za utafutaji huwa zinapungua kiasi. Muda si mrefu nimeingia mgahawani kwa ajili ya kupata breakfast.

Nilipofika, wahudumu walikuwa busy kiasi jikoni basi nikaamua kuendea meza ya vyombo ili nichukue kikombe nimimine chai.

Pembeni ya vikombe vya chai kuna kikombe kikubwa mithili ya jagi kimefunikwa na kimewekewa kitambaa chekundu juu, kitambaa ni safi kabisa.

Nikashawishika kukigusa kutaka kuangalia mule kumefunikwa nini. Aisee! Kuna bonge la chura kafunikwa humo. Nimerudishia tu nikaondoka kimya kimya.
 
Yawezekana ulichoandika ni kweli, tatizo staili yako ya uandishi imekaa kimasihara.
 
Ushirikina na biashara za bongo ni kama Pete na kidole
Kipindi fulani nilikua Morogoro mjini, kuna tubiashara langu ambacho ilikua inanilazimu kwenda kununua vitu asubuhi mapema
Ikawa Kila duka ninaloingia nakuta wanachoma udi, karibu maduka yote
 
Yaani ile taswira imeniacha na kichefuchefu sana maana nilizoea sana kwenda hapo ninapokuwa home tu bila mishe. Kila nikitaka kula nakumbuka ile kitu basi kichefuchefu balaa tupu!
 
Kuna sehemu hua napenda sana kwenda kupata msosi hasa weekend,
Ngoja nifatilie zaid
 
Ungechunguza na yale maji ya kuoshea vyombo. Labda nikujuze kidogo "vitu unavyoviona sivyo vilivyo"
 
Hizo story mtaacha kula migahawani shauri yenuu😂😂😂😂...mtapata story za hovyooo humuu mtapoteana
 
Wengine tumeshakula sana, tangu form one mpaka form six, Kisha miaka mitano ya chuoni, more than 10 years ya kula kwa mama ntilie
Sema nilikua sifuatilii sana maana ningeshindwa kula
 
Leo ni wikiendi na kwa kiasi kikubwa upande wangu mishemishe za utafutaji huwa zinapungua kiasi. Muda si mrefu nimeingia mgahawani kwa ajili ya kupata breakfast.

Nilipofika, wahudumu walikuwa busy kiasi jikoni basi nikaamua kuendea meza ya vyombo ili nichukue kikombe nimimine chai.

Pembeni ya vikombe vya chai kuna kikombe kikubwa mithili ya jagi kimefunikwa na kimewekewa kitambaa chekundu juu, kitambaa ni safi kabisa.

Nikashawishika kukigusa kutaka kuangalia mule kumefunikwa nini. Aisee! Kuna bonge la chura kafunikwa humo. Nimerudishia tu nikaondoka kimya kimya.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom