Konny Joseph
Senior Member
- Aug 28, 2016
- 118
- 199
Watu wengi wanafikiri ushirikina ni kuabudia mizimu na kwenda kwa waganga kutambika tu.
Lakini ukweli ni kwamba hata kumuhusisha mwanadamu na mambo yanayohusu kudura na uweza wa mwenyezimungu ni ushirikina vilevile.
Tena huu ndio ushirikina mbaya maana unahusisha dhati na uwezo wa mwenyezimungu katika kupangilia mambo yake.
Hata kama tunaamini kwamba watawala ndio wanaotetea ugari wetu,tuwe na mipaka tusifikie kuwahusisha na mipango na mamlaka za kimungu.
Nakumbuka Kipindi cha Magufuli,watu walidiriki kumpa sifa za kuwazidi manabii na watu wema.
Aiyekuwa Sheikh mkuu wa Dsm,Shkh Elhad Mohammed,alithubutu kusema Magufuli ni zaidi ya Mtume Muhammad.
Na aliekuwa waziri wa mambo ya ndani,Mh.Kangi Lugola ,alithubutu kusema kuwa Magufuli ni zaidi ya yesu,baada mda mchache akapigwa uwaziri wa mambo ya ndani.
Niwaombe watu tujiepushe na ushirikina,uchawa uwe na mipaka maana ukizidi tutaukosa ufalme wa mungu.