SoC03 Ushirikishwaji unapunguza Lawama toka kwa Wananchi

SoC03 Ushirikishwaji unapunguza Lawama toka kwa Wananchi

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
Joined
May 3, 2023
Posts
175
Reaction score
88
UWAJIBIKAJI ni moja kati ya misingi ya Utawala Bora ambapo kutekelezwa kwa msingi huu kwa ukamilifu ni kutekelezeka kwa misingi mengine ya Utawala Bora kama vile ufanisi na tija, kuzingatia matakwa ya wananchi, haki za binadamu na mengineyo. Ni wazi kwamba unapotekeleza majukumu yako ya kazi uliyopangiwa utakuwa unatekeleza misingi mengine ya Utawala Bora kwa vile ndani ya kutekeleza majukumu kunakuwa na mambo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine yanagusa misingi mingine na hivyo huleta athari kwa dhana nzima ya Utawala Bora.

Uwajibikaji mara nyingi huangaliwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku iwe serikalini, katika sekta binafsi au hata katika jamii. Mara nyingi jamii huangalia zaidi uwajibikaji katika taasisi za serikali kuliko taasisi nyingine. Katika suala kutekeleza dhamana aliyopewa. Uwajibikaji unahitaji kuhakikisha kwamba madaraka ya umma yawe ya kibusara na sio tu kwa mujibu wa sheria, bali pia yatumike kwa mujibu wa taratibu bora za kiutawala, ambapo watu, mamlaka na taasisi zote zitabeba dhamana kwa matokeo ya maamuzi au vitendo vyao.

Makala hii ya uwajibikaji imejikita zaidi kuangalia uwajibikaji katika sekta ya Maendeleo ya jamii na Ustawi wa jamii na zaidi katika madawati mbalimbali ya usuluhishi kuona namna watendaji wake wanavyotimiza majukumu yao ya kila siku. Madawati haya yanaweza ama kuwa machochezi ya migogoro ya kifamilia au uendelevu wa Watoto wa mitaani na matendo ya kijinsia yanayoendelea katika jamii. Kuanzishwa kwa idara hizi za maendeleo na ustawi wa jamii ni kwa lengo la kutatua matatizo na sio kuchochea ongezeko la matatizo.

Malalamiko ni mengi juu ya watendaji kutotimiza wajibu wao kutokana na sababu mbalimbali. Miongoni mwa sababu zinazotajwa katika kuchangia kupungua kwa uwajibikaji katika hizi idara ni pamoja na dharura za mara kwa mara za watumishi zikiwemo harusi, maziko, kuuguliwa, uchelewaji na utokaji kazini kabla ya wakati, utoro kazini, uvivu katika kazi, matumizi mabaya ya mitandao pamoja na rasilimali za Serikali na kufanyakazi kwa mazoea Pamoja na kutokutumia mbinu thabiti za utatuzi wa ustawi wa jamii. Hali hii pia huchangiwa na tabia ya muhali katika kufanya maamuzi. Ili kuondokana na hali hii na kujenga jamii yenye kuwajibika ipasavyo ni vyema kwanza kuacha kufanyakazi kwa mazoea,kuifanya kazi kwa ushirikiano,kimtandao na kupunguza dharura.

Uwajibikaji ni hali ya kiongozi au mtendaji kuwa tayari kujibu, kubeba dhamana na kutoa maelezo kwa wananchi juu ya maamuzi au matendo aliyoyafanya katika kutekeleza dhamana aliyopewa. Uwajibikaji unahitaji kuhakikisha kwamba madaraka ya umma yawe ya kibusara na sio tu kwa mujibu wa sheria, bali pia yatumike kwa mujibu wa taratibu bora za kiutawala, ambapo watu, mamlaka na taasisi zote zitabeba dhamana kwa matokeo ya maamuzi au vitendo vyao.

Makala hii ya uwajibikaji imejikita Zaidi kuangalia uwajibikaji katika sekta ya maendeleo ya jamii Zaidi katika madawati ya kutatua matatizo ya kijamii na kifamilia. Haja iliyopo ya wananchi katika mitaa na familia na migogoro ya kifamilia na malezi ipo haja kuwepo na watendaji wenye mtandao mmoja ili kuweza kuwa na maamuzi mamoja ya matatizo ya kimaendeleo na kiustawi katika wilaya husika.

Katika kuangalia uwajibikaji mambo kadhaa yamezingatiwa ili kupima uwajibikaji katika ustawi wa jamii, maendeleo ya jamii na madawati ya uwezeshaji huduma na usuluhishi.

1. Uwepo wa madaftari ya mahudhurio na maelezo kwa siku nzima na baada afua gani za kimaendeleo na kiustawi kwa Pamoja wakishirikiana na wadau wametekeleza.

2. Kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na kurekodi matukio na kumbukumbu za waliopatiwa huduma na ufuatiliaji wa mwenendo baada ya huduma, kuna usemi usemao “nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio mema kazini”. hivyo ili kuthamini utu hakuna budi kuwa na nidhamu.

3. Maafisa maendeleo na maafisa ustawi wengi hawana vitendea kazi hivyo mara zote hutegemea sehemu za dini, watu binafsi au mashirika katikakumfanya afanye kazi ipasavyo.

4. Kufanya kazi kwa mazoea na kuwategemea wadau pekee pasipo wenyewe kujisimamia na kupigania kuhakikisha masuala ya kiustawi na kimaendeleo yanapatiwa utatuzi endelevu hivyo basi mdau akikwama matatizo yanarudi palepale.

5. Ofisi za maendeleo na ustawi ziwe mfano wa kuwa na mbinu mbadala za matatuzi ya matatizo kwa haraka na weledi na pasipo kuwa utegemezi hata katika masuala madogo ya kibinadamu na kimaadili.

6. Kufuatilia mrejesho wa matendo ya watendaji, kuwa na mbinu jumuishi za takwimu, kuwa na mtandao wa utendaji kazi na taarifa ili kuepuka wasio stahiki kutumia nafasi za wastahiki.

Kwa ujumla suala la uwajibikaji ni muhimu sana katika kukuza Utawala Bora nchini kwani huu ndio msingi wa maendeleo ya taifa. Kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake kwa kufanyakazi kwa bidii na kujitolea uchumi wa nchi utakua na maendeleo kupatikana na kwa kasi. Uwajibikaji kwa watumishi wa umma ni jambo la lazima na linalowezekana, hivyo basi kila mtumishi wa umma atimize wajibu wake kwa kufanyakazi kwa kujituma na maarifa.

“Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu”, Yote hayo yanamaanisha umoja na ushirikiano ndio nguzo kuu katika maendeleo. Katika maendeleo yoyote yale ili yawe endelevu na yenye manufaa kama kusudio lake lilivyopangwa, kuna vitu muhimu lazima kuzingatiwa:

1. Ushirikishwaji ni miongoni mwa misingi ya Utawala Bora
a) Wataalamu wa masuala ya Utawala Bora wameugawa ushirikishwaji katika nyanja kuu mbili. ushirikishwaji wa kuwatumia viongozi ama walioteuliwa au kuchaguliwa.

b) ushirikishwaji wa moja kwa moja. Ushirikishwaji huu humpa uwezo mwananchi kushiriki moja kwa moja katika kubuni, kupanga na kuamua ikiwa ni pamoja na kutoa maoni Ushirikishwaji wa jamii ni chachu ya mafanikio. Aina hii ya ushirikishwaji ni nzuri kwani inamuweka karibu mwananchi na jambo au miradi inayotekelezwa katika jamii husika. Mwananchi hujiona ni sehemu ya jambo linalotekelezwa.

Ushirikishwaji katika maendeleo ya jamii unalenga zaidi kuwashirikisha wananchi husika katika shughuli zozote za kimaendeleo ili wachangie na kujaribu kupunguza vikwazo katika kufanikisha shughuli hiyo. Ushirikishwaji unaweza kuwa kutoa wazo la mradi au kutoa wazo katika nyanja tofauti zikiwemo mipango- mikakati, namna huduma zitakavyotolewa pamoja na mambo mengine yanayofanana. Serikali, viongozi na wawekezaji wanahitajika kuangalia upya suala la ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Baadhi ya watendaji Serikalini wamekuwa wazito sana katika kuwashirikisha wananchi katika miradi mbalimabali ya maendeleo hivyo kuifanya miradi hiyo isifanikiwe kama lengo lake lilivyopangwa. Hii inawafanya wananchi kutokuwa na mipango mizuri ya kuitumia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom