SoC03 Ushirikishwaji wa makundi maalumu katika sekta ya utalii

SoC03 Ushirikishwaji wa makundi maalumu katika sekta ya utalii

Stories of Change - 2023 Competition

Bright18

New Member
Joined
Jul 5, 2023
Posts
1
Reaction score
1
UTANGULIZI

A: 1. SEKTA YA UTALII.

Sekta ya utalii ni miongoni mwa sekta mama hapa nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, sekta hii huchangia takribani asilimia kumi na saba (17%) ya pato la nchi pia ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya ajira kwa rika zote kuanzia wamiliki wa makampuni ya utalii, watoa huduma kwa watalii (wasafirishaji na hoteli) hadi waongoza watalii kwenye maeneo husika.

2. FAIDA ZA SEKTA YA UTALII.

Licha ya kua na faida za maendeleo ya kiuchumi utalii huchangia kujenga afya ya mwili na akili kwa kusaidia mshiriki (mtalii) kupunguza msongo wa mawazo, utalii huchangia katika utunzaji na uendelezwaji wa rasilimali na vivutio vya nchi kuanzia wanyama pori, misitu na vyanzo vya maji, vile vile utalii kwa kiasi kikubwa unachangia uhusiano mzuri baina ya wageni na wenyeji na baina ya nchi na nchi.

B: MAKUNDI MAALUMU.

Watu wenye mahitaji maalum wapo wenye ulemavu wa kimaumbo, kiakili na kitabia kundi hili la watu wenye mahitaji maalumu wanaweza kupatikana majumbani na katika vituo vinavyotoa huduma za kuwatunza.

Kwenye jamii zetu za kitanzania na duniani kwa ujumla tunashuhudia ongezeko kubwa la watu wenye mahitaji maalamu ( watu wenye ulemavu) mwaka 2012 watu wenye ulemavu duniani walikua milioni 650 sawa na aslimia kumi (10%) kwa sasa kuna watu bilioni 1.3 sawa na asilimia kumi na sita (16%) ya idadi ya watu wote duniani.
Ongezeko hili la watu wenye mahitaji maalumu lina mchango mkubwa katika sekta ya utalii.
  • Haki za ushirikishwaji katika nyanja za kiuchumi na kijamii.
Kwa kuzingatia haki za binadamu watu hawa wenye uhitaji maalamu wana haki ya kuhusika ama kuhusishwa katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo na kijamii katika nchi yetu ikiwemo sekta ya utalii, kundi hili kubwa linaweza kunufaika na faida lukuki zinazo patikana kwenye sekta ya utalii kuanzia ajira (kipato) hadi faida za afya ya mwili na akili.
  • Sababu za kutoshiriki kwenye shughuli za kitalii.
Kwa muda mrefu kumekua na changamoto ya watu wenye mahitaji maalumu kushiriki katika shughuli za kitalii kuanzia ufanyaji kazi katika sekta hii hadi kushiriki kutembelea hifadhi na vivutio mbalimbali tulivyojaliwa kutokana na kutokuepo kwa miundombinu shirikishi au kwa kuepo kwa miundombinu mibovu ambayo siyo rafiki kwa watu wenye ulemavu.
  • Mapendekezo kwa serikali na wizara husika.
Kutokana na ongezeko la kundi hili kubwa ni vyema serikali kupitia wizara yenye dhamana wizara ya maliasili na utalii ikishirikiana na wizara ya afya na ustawi wa jamii pamoja na wadau wengine wa utalii, wanapaswa kufanya yafuatayo ili kuwezesha ushiriki wa watu wenye mahitaji maalumu kwenye sekta ya utalii;
  • Kutoa elimu kwa jamii kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye utalii;
Serikali kupitia wizara husika inawajibu wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu faida za kiuchumi, kiafya na kijamii juu ya ushiriki wa watu wenye mahitaji maalumu (walemavu) kwenye utalii katika uongozi hadi kutembelea vivutio na kushiriki michezo inayofanywa na watalii.
  • Kuboresha miundombinu na kuongeza vifaa shirikishi na wezeshi kwa watu wenye ulemavu;
Wizara ya maliasili na utalii pamoja na wizara ya afya na ustawi wa jamii zina wajibu wa kuanzisha miundombinu kama barabara kwaajili ya baiskeli za walemavu na kuweka vifaa vya kisasa vitakavyo wawezesha watu wenye mahitaji maalumu katika vivutio mbalimbali vya utalii, mfano kamba na fimbo rasmi katika kupanda milima.

  • Kuandaa matamasha makubwa kwaajili ya watu wenye ulemavu; Kwa kuandaa matamasha na majarida mbalimbali ya kitalii kwaajili ya watu wenye mahitaji maalumu yatasaidia kwa kiwango kikubwa kuhamasisha kundi hili kujitokeza kwa wingi na kuongeza ushawishi kwenye jamii na kushiriki katika shughuli tofauti tofauti za kitalii.
  • Serikali itenge bajeti maalumu kwaajili ya ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye sekta ya utalii; Bajeti hii itasaidia kuchochea ushiriki wa watu wenye mahitaji maalumu kwa kuandaa zawadi mbalimbali kwa washindi.
  • Mapendekezo kwa jamii (Tanzania)
Jamii za kitanzania zinapaswa kufanya yafuatato katika kuongeza ushiriki wa watu wenye mahitaji maalumu kwenye sekta ya utalii.

  • Kuacha mila ya kwaficha watu wenye ulemavu ndani;
Jamii zetu zimekua zikiwaficha watu wenye ulemavu na kuwanyima haki ya kushiriki katika matamasha mbalimbali kwa kuhofia aibu kwa familia na muda mwingine kuhusisha na imani za kishirikina.
  • Jamii izingatie kipaji na uwezo alionao mtu mwenye ulemavu;
Kwa kufanya hivyo tutaweza kuendeleza vipaji na uwezo binafsi wa wahusika ili kuleta tija katika nyanja ya utalii.
  • Ushauri kwa Jamii
Umuhimu wa shughuli za kitalii kama kupanda milima, kutembelea mbuga za wanyama, mashindano ya baiskeli mbugani, kupanda baloni ni kuwajengea watu wa kundi hili uwezo binafsi wa kujiamini na kuona mchango wao ndani ya jamii, nchi na dunia kwa ujumla pia inawasaidia kujiendeleza kiakili na kimaumbo (ukakamavu).
  • Maoni.
Kutokushiriki kwa watu wenye ulemavu katika shughuli za kitalii inawapelekea kupata uzito mkubwa, mashambulizi ya magonjwa mara kwa mara ukilinganisha na wale wanaoshiriki.

Mwisho, ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu ni muhimu uzingatie afya ya mhusika kwa ujumla, chaguo pekee analopendelea mshiriki, usalama wa shughuli husika, vifaa rasmi kwaajili ya kumuwezesha kushiriki.
Kwa kuwawezesha watu wenye mahitaji maalumu tunawajengea uwezo wa kutoa mchango wao na kua tegemeo ndani ya familia na taifa kwa ujumla.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom