SoC04 Ushirikishwaji wa Taasisi za kidini kwenye nyanja za kiuchumi na kimaendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

RK Ngunda

New Member
Joined
Jun 22, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Dunia ya sasa imekuwa ikitawaliwa na kushawishiwa na taasisi mbalimbali za kidini katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kielimu, kiuchumi na hata kijamii. Mwitikio na ushawishi wa taasisi za kidini umekuwa mkubwa kwa waumini wao ukilinganisha na ushawishi wa wanasiasa.

Mfano. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francisko ni miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa duniani kutokana na nguvu ya kiimani.
ILI KUIJENGA TANZANIA TUNAYOITAKA
1. Serikali inapaswa kutumia ushawishi wa viongozi na taasisi za kidini kufikisha sera, malengo na mikakati ya serikali katika kuijenga Tanzania katika nyanja mbalimbali.
2. Serikali iunde umoja wa viongozi wa kidini wenye lengo la kuwaunganisha viongozi wa kidini na uongozi wa serikali kujadili, kutathimini na kuweka sera na mikakati ya kuijenga Tanzania tunayoitaka.
3. Viongozi wa juu wa kidini nchini watumie ushawishi wao kutoa amri zenye sera, malengo na mikakati ya kuijenga Tanzania tunayoitaka
4. Taasisi za kidini zinapaswa kuwa na mafunzo ya elimu ya kujitegemea kwa waumini wao ili kulikomboa taifa kutoka kwenye anguko la utegemezi wa ajira serikalini. Hii itawafanya wananchi wengi kuwajibika na kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo bila kutegemea ajira serikalini.
 
Upvote 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…