Ni wajibu wa polisi kushirikisha wananchi katika shughuli za ulinzi na usalama wao na Taifa kwa ujumla. Hatua hii imekuwa ikileta matokeo chanya kwani ushirikiano huu huibua uhalifu ambao umejificha.
Polisi jamii ni moja ya mikakati iliyoanzishwa kwa lengo la kuwashirikisha wananchi katika masuala ya ulinzi na usalama.
Tafiti iyofanywa na chuo huria cha Uingereza 2020 imeeleza namna polisi jamii imeweza kusaidia kupunguza uhalifu katika Jiji la Mwanza. Huku mgongano wa vyama vya kisiasa ukitajwa kama chanzo cha mgawanyiko wa wananchi na kuathiri ushirikiano wa jeshi la polisi na wananchi.